Sunday, August 19, 2012

KUMPINGA KADHI SI KUJIUENGUA UISLAM TANZANIA

 SHEIKH  MOHAMED  MUSSA  ANATUNASIHI    -  19/8/2012

Re. Kumpinga Kadhi ni kujiengua Uislamu - Muft Simba

Assalaam laykum.
 
Kwanza nimshukuru sana kaka Hassan Msuya kwa majibu yake mazuri na ya hoja kwa dada Subrira. Nitangulize kusema kwamba kweli dada yetu Subira anaonekana ana uchungu haswa kuhusu maendeleo ya dini hii lakini pengine kwa kutokuwa "in the thin and thick of it" kida'wah hana ueledi wa mengi tu kuhusu Bwakata na taasisi nyingine za Kiislamu Tanzania na pia kwa kuwa anakiri kwamba "Waislam wengi tu wa nchi hii pamoja na mimi mwenyewe tumesoma dini yetu kwa kukaririshwa aya na sura za Qur'an, kukaririshwa maulid, Qaswida za kumsifu mtume, na namna ya kuswali. Ni wachache waliobahatika kupata elimu za fiqi na aqida kutoka kwa waalimu wao wa madrasa", kwa kukosa Ilmu hiyo ya Fiq-hi na Aqeedah, basi hawezi kuepuka kuwa na mtazamo huo alionao. Dada Subira hujachelewa, jitahidi kuitafuta eIlmu hiyo uliyokosa kuisoma huko nyumba kwani wenye Ilmu wanasema "Itlubuu al-Ilma min al mahdi ila al-llahdi" (Tafuteni elimu kutoka mbelekoni hadi kwenye mwandani (wa kaburi)". InshaaAllah utafanikiwa tu.
 
Naona na mimi niongezee hapo kwa nji aya kurejea hoja moja baada ya moja ya dada Subira nikitoa mchango wangu kuiunga mkono au kutofautiana nae.
 
1. Waislam wa Tanzania tulio wengi hatuna chombo mbadala kilichoundwa kisheria zaidi ya BAKWATA. Hii ni kwa sababu masheikh wanaojinasibisha na BAKWATA wapo kila mkoa, kila wilaya, Kata, Tarafa na kwingineko kila kijiji. Taasisi nyingine hazina mfumo huo.
 
Kaka Hassan amekujibu vizuri sana. Uislamu hauangalii wengi wako wapi bali haki iko wapi. Huo mtandao wa Bakwata ni moja ya kikwazo dhidi ya waislamu kwani ni rahisi adui kumwaga sumu yake juu ngazi ya taifa na ikaenea hadi kijijini. Kwa wenye kutaka mabadiliko, hawataogopa kuibadili hali hii eti kwa sababu masheikh wengi wanajinasibisha na Bakwata. Tukumbuke kuwa Bakwata si dini bali chombo tu kama taasisi nyingine. Tatizo letu wako waislamu (si wewe dada Subira) wamefikia kuiona Bakwata kama dini.
 
Amaa kuhusu taasisi nyingine kuw ahazina mtandao hadi vijijini, mwanawachuoni mmoja aishie Marekani alipata kuwaambi avijana waliomuuliza je, na ninyi mnao mtandao kama wa bakwata hapa Tanzania? Akawaambia, katika hali ya uadui wenye nguvu dhidi ya Uislamu kama wa Marekani, kuwa na mtandao mmoja hadi vijijini si hatari zaidi kuliko kuwa dispersed alimradi mnao uratibu wa pamoja. Hili humfanya adui awe na kazi kubwa kukabiliana nanyi. Aliuita muundo huu "Bush Fires" na kwa kuwa dada Subira ni mwana misitu mwenzangu, unajua hatari ya bush fires kwa maisha ya wanaoingi aporini kuuzima moto huo.
 
na stratejia hii ndiyo aliyoanza nayo Mtume (Swallah Allwaahu 'alayhi wasallam) alipoingia Madinah, hakuwa na standing army bali mobile units. Zikawapeleka pua mayahudi na ndiyo baadaye akawa na standing army. Hoja hapa si watu waendelee kuikumbatia Bakwata kwa kuwa ina mtandao mkubwa bali huo mtandao wenyewe ndiyo balaa kwa waislamu. KUNA WAKATI UNITED WE PRESENT THE ENEMIES WITH AN EASY TARGET, WE BECOME SEATING DUCKS.
2. Kila binaadam ana mapungufu yake, kumwita Mufti KAFIRI nadhani ni kosa kubwa sana kwake binafsi na kwa anaowaongoza hata kama ni vipofu katika dini yao.
 
Hapa nakubaliana nawe mia kwa mia kwamba "Ukamilifu ni wake Manani". lakini natofautiana na wewe kwa nukta hii "Uislamu umekataza kumuita muislamu KAFIRII pasina sababu za KiShariah". Kanuni hii itumike kw auadilifu kumhukumu Mufti wa Bakwata na kujihukumu sisi. Kama kuna mtu ameheshimiwa a waislamu hapa nchini Tanzania pasi ni Mufti wa Bakwata. Mufti huyu angekuwa say Uganda, Rwanda, Kenya n.k. yangekuwa mengine lakini watanzania na waislamu wa tanzania ni wastaarabu sana hadi mtu anaua-abuse ustaarabu wao.
3. Ukombozi kwa Waislam wa Tanzania hautapatikana kwa kukashifiana wenyewe kwa wenyewe.
 
Hapa dada Subira uko sahihi mia fil mia. Sina cha kuongeza zaidi ya kusema kashfa yenyewe ianishwe wazi ni ipi. Kwani Mufti wa Bakwata kuambiwa na masheikh wenzake amekosea kujipa mamlaka ya kuteua makadhi kwa ajili ya watanzania wote ni kashfa?
4. Bwana Simba ni binaadam kama mimi na wewe, ukidhani kuwa anapotoka ni vizuri kumkabili na kumwambia. huo ndiyo uislam.
 
Kwa hili kaka Hassan kanitosheleza kwa maelezo yake. Ni kweli tulisoma barua ya kuambiwa kwamba kwa kuteua maakadhi wa Bakwata na ku-extrapolate wawe wa waislamu wote wa Tanzania kakosea. Sasa nadhani ulimaanisha hili la jana kusema kwake "anayepinga uteuzi wake ni kafiri". Kwa hili nadhani masheikh wenzake watamwambia na kila mmoja wetu aanapaswa kumwambia. lakini dada Subira, hebu fikiria mimi na wewe tunamfikiaja Mufti Simba? Tena kama wewe si Bakwata ndiyo hautasikilizwa kabisa. Kama huamini naomba tukupe assignment umfikishie kwamba kakosea kuwaita masheikh zetu na wengine wanamzidi umri na IOlmu kwamba ni makafiri kwani wao ndio waliomwandikia barua kupinga uteuzi wake.
 
TAFADHALI DADA ICHUKUE ASSIGNMENT HII UMFIKISHIE MUFTI SIMBA KWAMBA WAISLAMU WENZIE WANASEMA AMEKOSEA KUWAITA MASHEIKH WENZAKE MAKAFIRI. Tunasubiri jibu utakalorudi nalo. Katika assignment hii utajifunza mengi sana, tafadhali jaribu.
 
5.Waislam wengi tu wa nchi hii pamoja na mimi mwenyewe tumesoma dini yetu kwa kukaririshwa aya na sura za Qur'an, kukaririshwa maulid, Qaswida za kumsifu mtume, na namna ya kuswali. Ni wachache waliobahatika kupata elimu za fiqi na aqida kutoka kwa waalimu wao wa madrasa. Na hii ndiyo iliyopelekea kulala na kudorora kwa Uislam na maendeleo ya Waislam.
 
Katika hili dada yangu "No comment". Umetoa analysis ya kisomi hasa.
6. Kuhusu Kadhi nafikiri tumepata pa kuanzia. Suala lisiwe hatutaki kadhi huyu bali liwe kuimarisha na kumfanya atambulike kisheria. Tusipokuwa makini mchakato wa maoni ya Katiba utapita tukiendelea kubishania kadhi aliyepo badala na kuhangaikia shuala hili kuingia kwenye Katiba.
 
Ama hili la kwamba "kwa uteuzi huu tumepata pa kuanzia, tusipinge bali tuimarishe ili kumfany atambulike kisheria", nikumbushe kwamba kwa background ya ilmju yako tunakupa udhuru. Labda nikukumbushe na pia wana-forum kwamba Jopo la Masheikh 25 ndilo lilikuwa nyenzo ya kufikia huko kwenye kutambulika kisheria. Sasa kama msingi huu imara umeshavunjwa na jambo liko mikononi mwa Bakwata ambayo inakuwa "remote controlled" kutoka kwenye "Mfumo", unapata wapi matumaini kwamba tutafika huko? Kule kuvunjwa msingi ule imar ani moja ya mikakati kuhakikisha hatufikii kuwa na mahakama imara, yenye kukubalika na waislamu wote na inayotambulika kisheria. Kinyume chake, kuupinga uteuzi huu kwa nguvu zetu zote ndiko kutakakorejesha treni kwenye reli.
 
Kuhusu khofu ya kutokuwa makini na mchakato wa katiba, dada Subira watu tuko makini. Tunajua wapi tumeshafika kuhamasisha waislamu na wapi bado. Tatizo lako (na pengine wengine) muda wenu ni wa ofisini na michango yenu ni kw anjia nyingine. hata hivyo tunashukuru kwa msisitizo.
7. Mwisho natoa rai kwa wenye elimu, waliojaaliwa kipaji cha kuelimisha umma kuingia ndani ya BAKWATA na kuleta mabadiliko kwa nia ya kuendeleza dini ya Haki.
 
Hili la wenye elimu kuingia ndani ya Bakwata limerudiwarudiwa kusemwa kwenye forum hii mara nyigni kwamba "you can't put the cart before the horse". Kaka Hassan kasema vizuri sana. Huwezi kubadili kitu kwa kuinga ndani ya Bakwata, waulize (kama ungeweza) akina marehemu Sh Muhammad Ali Al Bukhry, Burhani Mtengwa, Musa Mdidi na wengine waliotangulia mbele za haki, waulize waliohai waliowahi kuwa Bakwata kwa lengo hilo ulilolieleza dada Subira walifikia wapi? Ni muhali kutwaharisha najisi lakini ni vyepesi kutwaharisha nguo, sehemu au mwili ukiingi anajisi.
 
Maassalaam.

2012/8/18 Hassan KMsuya <hassan_msuya1980@yahoo.co.uk>
 
Dada Subira,
 
Nashukuru kwa maoni yako. Ila pengine umenielewa vibaya dada yangu. Hapana mahali nilipomwita Mufti wa Bakwata kafiri!!!! Nilichofanya ni kuhoji - kuwa leo Mufti kudai kuwa atakayempinga kadhi wake amejiengua kwenye Uislamu anataka tuamini kuwa waTZ hatukuwa waislamu kabla ya kuwa na kadhi? Na kama leo hii ndio anaona kuwa UISLAMU umerejea kwa kuwa kamteua kadhi ina maana hata yeye katika umri wake wote alikuwa sio Muislamu? Tafsiri yangu kwa kauli aliyotoa Mufti ni kwamba UISLAMU haupo kama hamna UKADHI! Hata hivyo haizuii mtu kutafsiri vingine au kukubaliana na Mufti kuwa atakayempinga kadhi wake ni kafiri!!!
 
Kuhusu taasisi nyingine kuundwa kisheria sina hakika kwamba una maana gani. Lakini kama una maana ya kusajiliwa si kweli - taasisi nying zilizopo zimesajiliwa. Ama una maana kuungwa mkono na serikali?  Kama ni hilo, naamini unajua kuwa ni kwa nini inaungwa mkono na serikali. Hili la sensa tu ni ushahidi - kwani yaelekea BAKWATA imeguswa kuliko hata serikali! Serikali na maadui wengine wa Uislamu hawajakashfu au kutoa matamko makali dhidi ya wale wanaopinga sensa waziwazi - lakini tayari baadhi ya BAKWATA wameshakuja na hoja za Al-shaabab na kutaka serikali iwashughulikie wanaopinga sensa!!Huyo Clement Mshana aliyetoa TAKWIMU FEKI ameongea kiungwana (japo huenda yaliyojificha kifuani mwake yakawa tofauti)  lakini angalia alichoongea Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye kipindi hicho cha JAMBO. Issue hapa ni kwamba serikali au maadui wengine hawana sababu ya kutumia misuli kuonyesha dhahiri ubaya wao dhidi ya waislamu wakati wana chombo chao kinachoweza kutumika kufikisha ujumbe na hivyo kufanikisha malengo yao dhidi ya waislamu.
 
Ama kuhusu kukosa mitandao vijijini, nadhani suluhu sio kuhamasisha watu kuingia BAKWATA!! Dada yangu sio rahisi kiasi hicho. Ungeshauri kuwa taasisi nyingine zijiimarishe vijijini. Walioiunda BAKWATA hawatakubali ife kwa sababu iliundwa kwa malengo maalum. Dada yangu hujiulizi kwa nini serikali na kanisa lishughulishwe sana na BAKWATA, hasa inapokuja kwenye chaguzi zake. Hivi huna habari kuwa BAKWATA imewahi kuchangiwa na serikali na maaskofu ili kufanya uchaguzi wake? Ni kweli hao maaskofu wana nia nzuri kiasi hicho na waislamu? Kwa hiyo dada yangu naona kuingia BAKWATA ni mtihani! Wapo watu wasafi sana ndani ya BAKWATA  lakini hawafurukuti. Ndio maana leo katibu mkuu atasema hili kesho  Sheikh wa Dar es Salaam anaonekana kwenye vyombo vya habari akipinga! Ni kweli kuwa BAKWATA bado ina mtandao mkubwa. Lakini pia ni kweli kuwa BAKWATA inaendelea kufa. Nakumbuka wakati Kirinjiko Islamic inajengwa Masheikh wa BAKWATA kule upareni walikuwa busy kukataza waislamu kushiriki katika matamasha wakidai kuwa hao sio waislamu. Leo hii wazee hao hao hawafikirii kuwapeleka watoto wao Kibohehe, Bondeni nk. bali Kirinjiko!!
 
Dada yangu; unashauri kuwa kama naona kuwa Mufti amepotoka nimkabili nimwambie. Je, kwa Fatwa yake kuwa anayempinga kadhi wake ni kafiri (amejiengua kwenye uislamu) unaiona kuwa ni sawa?  Kama unakubaliana nayo sina tatizo na hilo. Ila kama hukubaliani nayo nikuombe wewe umkabili umwambie! Mara ngapi Mufti kaambiwa ikiwa ni pamoja na barua ya wenzake waliokuwa pamoja katika mchakato wa mahakama ya kadhi na waislamu kuonyesha wazi kushangazwa na hili la uteuzi wa KADHI lakini majibu yake ni hayo kuwa wanaompinga kadhi wake wamejiengua kwenye uislamu. Aambiwe nini tena hapo Dada yangu? 
 
 
Nadhani Dada Subira umenielewa na naamini sijakukera! Najua na naelewa uchungu ulio nao juu ya Uislamu. Lakini ndio hivyo -changamoto hazikosi!
 
Masalaam,
Hassan
 

From: subira sawasawa <siasawasawa@yahoo.co.uk>
To: tz_muslim_community@yahoogroups.com
Sent: Saturday, 18 August 2012, 2:41

Subject: Re: [tz_muslim_community] Re. Kumpinga Kadhi ni kujiengua Uislamu - Muft Simba
 
Sheikh/Ustadh/Maalim Msuya,
 
Pamoja na kwamba siiungi mkono BAKWATA naomba kutofautiana na wewe kama ifuatavyo:-
 
1.    Waislam wa Tanzania tulio wengi hatuna chombo mbadala kilichoundwa kisheria zaidi ya BAKWATA. Hii ni kwa sababu masheikh wanaojinasibisha na BAKWATA wapo kila mkoa, kila wilaya, Kata, Tarafa na kwingineko kila kijiji. Taasisi nyingine hazina mfumo huo.
 
2.   Kila binaadam ana mapungufu yake, kumwita Mufti KAFIRI nadhani ni kosa kubwa sana kwake binafsi na kwa anaowaongoza hata kama ni vipofu katika dini yao.
 
3.   Ukombozi kwa Waislam wa Tanzania hautapatikana kwa kukashifiana wenyewe kwa wenyewe.
 
4.    Bwana Simba ni binaadam kama mimi na wewe, ukidhani kuwa anapotoka ni vizuri kumkabili na kumwambia. huo ndiyo uislam.
 
5.  Waislam wengi tu wa nchi hii pamoja na mimi mwenyewe tumesoma dini yetu kwa kukaririshwa aya na sura za Qur'an, kukaririshwa maulid, Qaswida za kumsifu mtume, na namna ya kuswali. Ni wachache waliobahatika kupata elimu za fiqi na aqida kutoka kwa waalimu wao wa madrasa. Na hii ndiyo iliyopelekea kulala na kudorora kwa Uislam na maendeleo ya Waislam
 
6. Kuhusu Kadhi nafikiri tumepata pa kuanzia. Suala lisiwe hatutaki kadhi huyu bali liwe kuimarisha na kumfanya atambulike kisheria. Tusipokuwa makini mchakato wa maoni ya Katiba utapita tukiendelea kubishania kadhi aliyepo badala na kuhangaikia shuala hili kuingia kwenye Katiba.
 
7. Mwisho natoa rai kwa wenye elimu, waliojaaliwa kipaji cha kuelimisha umma kuingia ndani ya BAKWATA na kuleta mabadiliko kwa nia ya kuendeleza dini ya Haki.--- On Sat, 18/8/12, Hassan KMsuya <hassan_msuya1980@yahoo.co.uk> wrote:

From: Hassan KMsuya <hassan_msuya1980@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [tz_muslim_community] Re. Kumpinga Kadhi ni kujiengua Uislamu - Muft Simba
To: "tz_muslim_community@yahoogroups.com" <tz_muslim_community@yahoogroups.com>
Date: Saturday, 18 August, 2012, 9:43

 
Sheikh Muhammad Issa,

No comments:

Post a Comment