Friday, November 30, 2012

MHADHIIRI IMAN PETRO AFARIKI DUNIA DAR ES SALAAM, TANZANIA

Kwa mujibu wa taarifa niliyoipokea kutoka kwa mjumbe wa BARAZA KUU la Jumuiya na Taasisi za Kiislam,
Br. Ally Mbaruku
Ndugu yetu katika Iman,

IMAN  PETRO  AMEFARIKI  LEO JUMATATU NOV 26, 2012, BAADA YA SWALA YA MAGHARIBI,

Taratibu za maziko sikuzipata, anaejuwa atujulishe tafadhali
 
Marehemu katika uhai wake alikuwa na juhudi kubwa ya Dini
Aliwahi kurudishwa Bara kutoka Zanzibar kwa nguvu za Dola
Iman Petro ni mtu aliesilimu akitokea katika Ukristo, na aliugua ugonjwa usiojulikana kwa muda kiasi,

Baadhi ya Wahadhiri wanahisi kaumizwa na sumu kutoka kwa maadui wa Dini ya ALLAH, Maana Lecture  zake zilikuwa TISHIO
Tumuombe Mwenyezi Mungu amghufirie dhambi zake ndugu yetu na amtie katika pepo yake
 
 
INNAA LILLAAHI WA INNAA ILAYHI RAAJIWUUN
Wasalam
Pazi Mwinyimvua

UTEKELEZAJI WA "EVANGELIZING MUSLIMS" NCHINI TANZANIA

On Nov 27, 2012 4:22 PM, "Mohamed Issa" <hemedshk@gmail.com> wrote:
 

Assalaam alaykum.
 
Allah anatuambia katika Qur'an "Na hawatoacha kukupigeni vita mpaka wakuritadisheni kutoka kwenye dini yenu wakiweza.." (Al Baqarah 2:217)

Siku ya Jumamosi terehe 24 Novemba, 2012 itaingia katika maisha yangu ya da’wah kama siku niliyoona kivitendo jinsi ambavyo mipango iliyowekwa na wakristo kupitia mafunzo maalum yaitwayo “Evangelizing Muslims” inavyoweza kuwatoa waislamu kutoka katika Uislamu wao.

Nilialikwa kuhudhuria sherehe za ufungaji wa shule ya Kiislamu Iqra English Medium School inayoendeshwa na Pahi Islamic Center, taasisi iliyosajiliwa yenye Makao yake Makuu kijiji cha Pahi, Tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa yenye waislamu takriban 95%. Kondoa kuna vijiji huwezi kukuta mkristo hat ammoja lakini hivi sasa kuna kasi kubwa ya kuwaritadisha waislamu.

Ninaambiwa kwamba mnamo miaka ya 1998-2000, walifika wazungu watatu wakiwemo Wamarekani wawili (wanawake) na Mjerumani mmoja. Walifika wakidai kutaka kujifunza lugha na mila za kabila la warangi. Wakapokelewa na ndugu mmoja aitwaye Halifa Nchasi (ambaye sasa ndiye Katibu wa Pahi Islamic Center) na ndugu huyu akawafundisha hawa wazungu kirangi kwa muda wa wiki tatu na wakakimudu vizuri (walikuwa wataalam wa lugha).

Wale wanawake walifikia kuishi maisha ya mwanamke wa kawaida wa kirangi wakishiriki shughuli zote zifanywazo na mwanamke wa kabila hili kuanzia kuteka maji, kukata kuni hadi kubeba mtoto mgongoni na wakapewa majina ya kirangi-mmoja akiitwa Mwasu na mwingine Sware. Baada ya muda, jamaa hawa wakaja kuanzisha mradi uitwao “COMPASSION” ambao ulilenga kuwasaidi awaislamau masikini husuusan katika huduma ya afya.

Wakaanza kumimina misaada kutoka huko ughaibuni wakianzia na kuweka magari matatu katika vijiji vitatu- moja pahi kwenyewe, jingine Kinyasi na jingine Salare kwa ajili ya kubeba wagonjwa kwa kila mwenye mgonjwa kuchangia fedha ya mafuta tu Sh 10,000 kuepelekewa mgonjwa wake hospitalai ya Wilaya Kondoa mjini kwani tarafa nzima ya pahi haina hospitali. Wapashajai ahabari wangu wananiambia kwamba mara baada ya waazungu hawa kuja Pahi, malaria ya ajabu ilizuka. Wanaamini kwamba wazungu hawa walipandikiza mbu mwenye vimelea vya malaria.

Baadaye wazungu hawa wakaomba kupataiwa ekari 7 ili wajenge zahanati hapo Pahi. Uongozi wa serikali ya kijiji ukaitish amkutano wa hadhara na kuwataka ushauri wanakijiji ambao 99% ni waislamu. Kutokana na “wema” waliofanyiwa, wanakijiji wote wakaunga mkono wakristo hao kupatiwa ardhi waliyoomba. Wakrsito wakajenga zahanai yao na ikawa pia andiyo kituo cha kuwakusanya wale waislamu masikini kwa ajili ya mafunzo maalum kila jumamosi ambapo wakitoka huko hupatiwa mche wa sabuni, madaftari n.k.

Kilichofuatia ni jamaa kuomba atrdhi nyingine ekari 7 kwa ajili ya kujenga shule ya wasichana. Hivi sasa wanaendesha shule ya wasichana (boarding na day) yenye kuchukua wasichana 600 na kila mwaka ninaambiwa takriban wasichana waislamu 5-10 huritadi. Hata wale amabo hawajaritadi, huonesha wazi kuwa wameugura Uislamu kwa sababu wanapopita njiani wakawaona waislamu husuusan akina mama waliojisitiri husikika wakisema “Mashetani hao”.

Kubwa zaidi hiyo COMPASSION imeanzisha mtindo wa “Family Friends” ambapo familia moja masikini ya kiislamu huunganishwa na familia ya kikristo huko Ulaya ana Marekani na hiyo familia ya nje huisaidia familia ya ndani kwa hali na mali. Hili nalo limezidisha hatarii ya waislamu kuritadishwa na tayari familia kadhaa zimesharitadi familia nzima.

Kibaya zaidi, waislamu hapo Pahi wamegawanyika wakipigana vita. Answar Sunnah wamegawika makaundi mawili yenye kupingana na hawa wanaosema wao ni Bakwata pia ni faraqa tu. Hali ya Paahi na vijiji vingi vya Kondoa ni mbaya. Kingine cha kuzingatia Kondoa sasa ni Jimbo la Kanisa Katoliki lenye Askofu wake kamili.

Nimefanya fikra na waislamau pale na ndugu zetu wa Morogoro kwa ajili ya kuunusuru Uislamau pale. Yapo yaliyoazimiwa ambayo siwezi kuyaweka bayana humu bali niwatangazie tu biashara kwamba wale wenye Ilmu wanaaweza kuitembelea Pahi na kufanya da’wah. Pia wale ambao hatuna Ilmu, ikifikia wakati nguvu zikahitajika nasi tuwe tayari. Pahi imetengewa Tshs 10,000,000 kila mwaka kwa ajili ya kuritadisha waislamu.

Inasemekana wazungu hawa walisoma kwenye Mtandao kwamba Paahi ni Markaz Kuu ya Fisabiylillahi Marakaz barani Afrika. Ni kweli pahi kulifunguliwa Markazi Kuu ya Fiysabiilillahai Afrika mwaka 1981. Hadi sasa kuna ekari 110 zimekaa tu pasina kutumika mbali na msikiti uliowekwa jiwe la msingi na aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo Mzee Aboud Jumbe. Huu naoa ni udhaifu mkubwa wa taasisi hiyo. Pia kuna taasisi nyingine iitwayo IDA inazo ekari 16 nazo zimelala pasina kufanayika chochote hapo kwa miaka sasa. Watu wako tayari kinachokosekana ni uongozi na maelekezo.

Huu ni mfano tu kwani najua hali ndiyo hii sehemu kubwa ya nchi. Ukizingatia kwamba wakristo wana hiyo MoU yao na Serikali kutengewa mabilioni kwa ajili ya elimu, afya na huduma nyingine za jamii, bila shaka kasi ya kuwaritadisha waislamu itaongezeka.

--
Sheikh Muhammad Issa
(Private Mail)
Youtube Channel" Mohamed Issa

Sunday, November 18, 2012

MGOGORO WA DINI WAKIMBIZA MKUU WA SHULE BAGAMOYO SEKONDARI, TANZANIA

Imebandikwa hapa leo hii tarehe 18/11/2012.

Mgogoro wa dini wakimbiza Mkuu wa shule, wanafunzi


Na Thobias Mwanakatwe,  NIPASHE.
2nd November 2012

Mgogoro mkubwa umeibuka katika Shule ya Sekondari ya Bagamoyo mkoani Pwani kati ya wanafunzi wa Kiislamu na Kikristo na kusababisha Mkuu wa Shule hiyo, Bonus Ndimbo kuikimbia shule na familia yake kuhofia usalama wa maisha yake.  Pia, baadhi ya wanafunzi wa Kikristo wamekimbia shule hiyo na kurejea majumbani mwao kutokana na vitisho wanavyopewa. 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salehe Mbaga, akizungumza na NIPASHE jana kwa simu, alithibisha kuwepo kwa mgogoro huo, lakini alisema hajapata taarifa za kukimbia kwa Mkuu wa Shule
“Kama kweli Mkuu wa Shule amekimbia shuleni atakuwa amefanya vizuri kwa sababu alikuwa hatakiwi na wanafunzi,” alisema Mbaga ambaye hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi chanzo cha mgogoro huo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alipotafutwa, alisema mgogoro huo upo, lakini alikataa kutoa maelezo zaidi na hatua zilizochukuliwa yatolewe na  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.  Hata hivyo habari zilizopatikana shule hapo zinaeleza kuwa mgogoro hu ulianza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa serikali ya wanafunzi.   Wakati wa uchaguzi huo walijitokeza wagombea wawili wa nafasi ya Kilanja Mkuu wa Shule, Answal Abdul na Emmanuel Mmari ambao walikuwa wakichuana nafasi hiyo. Wote ni wanasoma kidato cha tano.  

Chanzo cha habari kinaeleza kuwa kampeni zilipoanza wanafunzi waKiislamu ambao baadhi yao ni viongozi wa msikiti uliopo shuleni hapo, walianza kumpigia kampeni mgombea wa dini yao na wa dini ya Kikristo walianza kufanya hivyo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa wakati kampeni zikiendelea, inadaiwa Mkuu wa Shule aliwasihi wanafunzi wa Kiislamu waache kupiga kampeni kwa kufuata misingi ya dini.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Shule inadaiwa iliwakera wanafunzi wa Kiislamu ambao walichukua uamuzi wa kumuondoa katika kinyang’anyiro mgombea wao waliyekuwa wakimpigia kampeni, Answal Abdul na kubakia mgombea pekee Emmanuel Mmari.

Habari zinaeleza kuwa siku ya uchaguzi wanafunzi wote walishiriki, lakini wanafunzi wa Kiislamu licha kupewa karatasi za kupigia kura hawakuandika chochote katika karatasi hizo huku wanafunzi wa Kikristo wakipiga kura.

Baada ya uchaguzi huo, Mmari alichaguliwa kuwa Kiranja Mkuu wa shule hiyo.Mkuu wa Shule hiyo, Ndimbo baada ya kukamilika uchaguzi huo alitangaza siku ya kuapisha viongozi wa serikali ya wanafunzi waliochaguliwa na ndipo mgogoro ulioanza.

Siku ya kuapisha viongozi hao, wanafunzi wa Kiislamu inadaiwa walimvamia Mkuu wa Shule na kumnyang’anya karatasi zilizokuwa zimeandikwa majina ya viongozi waliopangwa kuapishwa,  hali iliyozua vurugu ambazo hata hivyo, baadaye zilitulia.

Mtoa habari watu amesema tangu siku hiyo wanafunzi wa Kiislamu walianza kushinikiza Mkuu wa Shule ahamishwe na kwamba hawautambui uongozi wa shule uliochaguliwa na pia hawataki walimu Wakristo shuleni hapo.

Habari zaidi zinasema kuwa vitisho viliendelea na kuwa nyakati za usiku watu wasiofahamika walikuwa wakipita na pikipiki kuzunguka mabweni ya shule.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi wa Kikristo waliamua kuondoka shuleni hapo kurejea majumbani hadi sasa kuhofia usalama wa maisha yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Samuel Saliyanga, alipoulizwa alisema bodi ya shule hiyo ilikuwa inakutana jana kutoa maamuzi ya suala hilo na kwamba yeye atapata taarifa kupitia kwa Afisa Elimu ya Sekondari.

CHANZO: NIPASHE

PHILADELPHIA, U.S.A. MALE RESIDENTS SPORTING BEARDS !!!

Posted here on  18/11/2012. 

BEARDS  A  STYLE STATEMENT IN PHILADELPHIA,  U.S.A.

There’s not a woman in Philly who would rock a burka just to make a fashion statement.
But when it comes to Muslim-inspired menswear, well, that’s another story. Regardless of their religious affiliations, certain Philadelphia men, mainly African-Americans, have adopted the style of wearing long, old-world-style beards, sometimes pairing them with calf-length trousers and long shirts – all looks inspired by traditional Muslim attire.
For many, this convergence of hip-hop with Islamic style is purely a fashion statement and has nothing to do with whether a guy worships in a church or mosque. Some jokingly refer to non-Muslims who adopt this mode of dress as “asalama-fakems,” a play off the traditional Arabic greeting of “as-salaam alaikum,” meaning “peace be upon you.”
Whatever you call it, the Islamic-style aesthetic has been around for a while, and the beard in particular – often referred to as a “Philly beard” or a “Sunni” – has come to be identified with the City of Brotherly Love. My friend Anthony Henderson, the fashion stylist who divides his time between Philly and Los Angeles, makes a point of wearing it because of hometown pride.
“I can go to a corner store in Crenshaw or in Watts and people will say, ‘You’re from Philly,’ ” Henderson said. “And if I have to go to a new barber here in Los Angeles, I say, ‘I need a Philly beard.’ They automatically know what it is.
“I love my Philly beard because I think it makes me look attractive and sexy. People like to touch it and pull on it.”
Henderson’s chin whiskers are in a circle beard that connects his mustache with his goatee, and are darkened with hair dye that gives his beard Philly-esque definition. Barbers such as Darryl Thomas of Philly Cuts at 44th and Chestnut will use a dark wax pencil to give a sharp edge to the beard, a “serious outline.”
“We just put that razor on it and make it look real hot,” Thomas told me.
The most famous Philly beard-wearer is rapper Freeway.
“In college, we would often call it the Freeway beard, the Philly beard or the Muslim beard, also the West Philly beard,” said Ben Piven, who created a short YouTube documentary on the topic. “There’s a specific shaping to it, the way it puffs out around the cheeks and the sideburns and extends below the chin, definitely low in the mustache area in keeping with the Islamic style of facial hair.
“It’s definitely well-groomed, well-kept. It’s a neat look,” he added.
To the uninitiated, the trend can confuse. When Adnan A. Zulfiqar, the Muslim spiritual adviser at the University of Pennsylvania, moved here in 2003 to study law, he would automatically give the Muslim greeting of peace to Philly beard-wearers, assuming that they, too, were conservative followers of Islam. According to tradition, devout Muslims trim their mustaches but allow their beards to grow.
“Muslims will wear the beard as a way to pay respect to the prophet Muhammad. Muslims believe that all the Abrahamic prophets wear beards,” Zulfiqar told me. “It’s a sign of piety. It’s a sign of religiosity, a sign that you’re trying to walk the path that the prophet walked.”
He added, “I think a lot of people in Philly do it because it’s become a part of the culture, urban culture in particular. It’s now part of Philly.”
Zulfiqar occasionally will be approached by a stranger who compliments him on his facial hair by saying, ” ‘I like your Sunnah.’ ”
“Sunni” is derived from the term Sunnah, which is Arabic and generally refers to the practices or ways of the prophet Muhammad. Police dispatchers can be heard on police scanners describing suspects as wearing “Sunni” beards.
The so-called Philly beard has been growing in popularity with non-Muslims since the mid-’90s, according to Mark Lightfoot, owner of the Philadelphia Hair Co., 5805 Germantown Ave.
“It probably started out as a fad, but it’s not dying down,” said Lightfoot, who’s also a barber. “If it’s 10 people I do, it’s probably six or seven of them that get it.”
The popularity of the beards is a sign of how mainstream Muslim culture has become in Philadelphia. Another example is the style of wearing pants cropped to an above-the-ankle length. During ancient times, certain Muslims would allow their clothing to drag on the ground as a sign of extravagance or to demonstrate their wealth.
“More conservative Muslims believe your pants shouldn’t be below your ankles because it’s a sign of arrogance,” explained Zulfiqar, who’s working on a doctorate in Near Eastern languages and civilizations. “The prophet was, like, ‘No. You have to be simple.’ ”
Given the number of Muslims in Philadelphia, this look is likely to endure.
But the beard? Like a lot of women, I much prefer a little chin stubble to a full-face beard. I asked Thomas of Philly Cuts if he thinks that the Philly beard will ever go out of style, and he laughed.
“They are here to stay. This is Philly. You don’t see the cheesesteak going anywhere. You don’t see the hoagie going anywhere. This is what we do.”
Source
http://muslimvillage.com/2011/08/24/13211/the-sunnah-beard-the-latest-trend-amongst-non-muslims-in-philadelphia-usa/

Mtaa wa UGOMBOLWA, KATA YA SEGEREYA, WILAYA YA ILALA, DAR ES SALAAM, TANZANIA, WAFUNGA MACHINJIO YA NGURUWE,

Ugombolwa wafunga machinjio ya nguruwe
 
na Betty Kangonga
 
Tz Daima 18 Nov 2012
 
UONGOZI wa Serikali ya Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala, imeyafunga machinjio ya nguruwe kutokana na wamiliki hao kukiuka taratibu za kisheria.
Akizungumza jana mara baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika machinjio hayo yaliyopo katika eneo la makazi, Ofisa Mtendaji wa mtaa huo, Mathew Mayonga aliyeambatana na uongozi wa mtaa huo, alisema amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha na ukiukwaji wa taratibu.
Alisema kuwa amelazimika kuyafunga machinjio hayo na kuwasilisha zuio la mahakama kutokana na uongozi wa mtaa huo kutokuwa na taarifa juu ya uwepo wa machinjia hayo katika eneo hilo.
“Yaani naomba kuanzia sasa msimamishe zoezi la uchinjaji na muuze nyama zilizokwisha andaliwa…na kama mtakiuka utaratibu huo nina hakika nitapata maelezo na hapo ninajua nini hatua ya kuchukua,” alisema.
Mayonga, alisema kuwa wamiliki hao hawana nyaraka zozote zinazowahitaji kufanya shughuli hiyo hivyo hata uandaaji wa nyama hiyo unaweza kuwa na dosari.
Alisema baada ya kukagua mazingira yanayolizunguka eneo hilo alibaini utitirishwaji hovyo wa maji machafu ambao umekuwa kero kubwa kwa majirani wanaoishi eneo hilo.
“Mnawezaje kufanya kazi wakati hakuna nyaraka zinazowataka kufanya hivyo kwa kweli naomba msimamishe haraka hadi mtakapopata barua rasmi la kutakiwa kufanya shughuli hiyo,” alisisitiza.
Naye Mwenyekiti wa mtaa huo, Mariam Machicha, alisema kuwa hiyo ni mara ya pili kufika katika eneo hilo na mara ya kwanza walilazimika kulifungia eneo hilo lakini wakashangaa kwa kufunguliwa tena.
“Hii ni mara ya pili nafika hapa…mara ya kwanza tulilifunga lakini cha ajabu likafunguliwa kinyemela,” alisema
Akijitetea Katibu wa Umoja wa wadau wa nguruwe Manispaa ya Ilala, Daudi Charles, alisema kuwa ofisa mifugo wa wilaya hiyo aliwataka kuendelea na biashara hiyo huku akiendelea kuwatafutia vibali.
 

Saturday, November 17, 2012

MUHARRAM NA MASHIA

 Imebandikwa hapa leo hii 17/11/2012.
 
Assalaam alaykum.
 
Umekurubia kuingia mwezi wa Muharram, miongoni mwa miezi mitakatifu katika Uislamu iliyofuatana ambayo ni miwili kabla ya huo ujao (Dhul Qaadah na Dhul Hajji) na kisha mwezi wa Rajab. Katika mwezi huu wa Muharram, Mashia au Rawaafidhwah hufanya sherehe zao za masiku kumi ya Muharram ziitwazo Sherehe Ashuura.
 
Mashia wanaitwa pia Rawaafidhwah kwani jina hili kalitaja mmoja wa ma-Sheikh wao Almajlisy katika kitabu chake (Bihaarul-anwar) akasema katika mlango aliouita, mlango kuhusu ( Ubora wa raafidhwa na uzuri wa kujiita jina hili), kisha akataja kutoka kwa Sulaiman Al-aamash kuwa amesema: niliingia kwa Abii Abdillah Jaafar bin Muhammad nikasema kumwambia: Hakika watu wanatuita Raafidhwa, nini maana ya Raafidhwa? Akasema: wallwahi sio wao waliokuiteni hivyo bali Mwenyezi Mungu alikuiteni hivyo katika Taurati na Injili kupitia ulimi wa nabii Mussa na nabii Issa.( Tazama kitabu (Bihaarul-anwar) cha Almajlisy 65/97. (ambacho ni miongoni mwa marejeo yao muhimu katika vitabu vyao vya sasa)
Na imesemekana kuwa: wameitwa raafidhwa kwa sababu walikuja kwa Ally bin Hassan wakamwambia: Jitenge na Abubakari na Omar ili tuwe pamoja nawe, akasema: wao ni vipenzi wa Babu yangu, siwezi kujitenga nao bali niko pamoja nao, wakasema: hivyo basi tumekukataa, ndipo wakaitwa Raafidhwa, na akaitwa kila aliyemuunga mkono Zaid kuwa ni Zaydiyya.(Rejea: Attaaliqaat alaa matni lum-atul iitqaad cha Sheikh Abdallah Aljibriin uk.108).

Na inasemekana:wameitwa Raafidhwa kwa kupinga kwao utawala wa Abubakari na Omar (Radhi za Allwah ziwe juu yao) -Tazama Maqaalaatul-Islaamiyiin cha muhyiddiin Abdulhamiid (1/89) na imesemekana: Wameitwa hivyo kwa kukataa kwao Dini. (Tazama Ibid 1/89)
Kwa hiyo Mashia au Rawaafidhwah ni pote jengine kabisa mbali na Ahlu Sunnah wal Jamaa lakini waislamu wengi wanaojinasibu na Ahlu Sunnah wal Jamaa wamekumbwa na itikadi za Kishia na miongoni mwa hizo ni sherehe zao za Ashuura katika mwezi huu wa Muharram ambapo hukumbuka kifo cha Al Hussein Ibn Ali (Radhi za Allwah ziwe juu yake na Baba yake pia). Shubha inayopataikana hapa ni kwamba siku ya Ashuura imethibiti kwa hadithi za Mtume (Rehma na Amani ziwe Juu lake) alopofika Madinnah ana kuwakuta Mayahudi wakiadhimisha siku hii ambayo ni terehe 10 Muharram. Akawauliza ni siku gani hii mnayoiadhimisha? Wakasema ni siku Allwah alipomuokoa Musa na watu wake dhidi ya Firauni. Mtume akawaambia sisi ndio bora kwa Musa kuliko nyie. Hapo Mtume (rehema na amani ziwe juu yake) akamuarisha swahaba awatangazie watu kuwa yeye atafunga swaumu siku hiyo na iliyo kabla yake yaani "Yawmu Taasu'a". 
“Ashura”: Hii ni ile siku ya mwezi kumi Muharram (Mfunguo nne) na “Taasuaa”: Hii ni siku ya mwezi tisa Muharram. Dalili na ushahidi wa usuna wa kuzifunga siku mbili hizi ni ile hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Abbas-Allah awawiye radhi-“Kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alifunga siku ya Ashura na akaamrisha watu kufunga”. Bukhaariy [1900] & Muslim [1130]-Allah awarehemu.

Kwa hiyo kilicho Sunnah ni kufunga siku ya tarehe 9 na 10 Muharram kama alivyofanya Mtume (Rehma na amnai za Allwah ziwe juu yake) kinyume na wafanyavyo Mashia/Rawaafidhwah wafanyavyo kwa kuzifanya siku hizi za vilio na kujipiga miili hadi kutoka damu eti kwa kukumbuka kuuwawa kwa al Hussein Ibn Ali (Radhi za Allwah ziwe juu yake na baba yake Ali Ibn Abi Twaalib).
Itikadi za Mashia kuhusu kuuwawa al Hussein ibn Ali (ambazo ndiyo chimbuko la Sherehe zao za Ashuura/Muharram) zimewafikisha hata kukufuru juu ya Allwah na matukufu yake. Kwa mfano, Mashia wanaitakidi sehemu yalipo makaburi ya watu waliodai kuwa ni maimamu wao, au ambao ni maimamu kweli, kwa sehemu hizo ni sehemu takatifu,hivyo Alkuufa ni haram(sehemu takatifu),pia Karbalaa ni haram,na Qumm nayo ni haram. Na wanayo riwaya wanayo dai kuwa imepokelewa kwa Asswaadiq kwamba, Mwenyezi mungu anayo haram yake ambayo ni makka,na Mtume wake anayo haram yake ambayo ni Madina,na amiiril-mu`uminiina anayo haram yake ambayo ni Alkuufa,na sisi tunayo haram yetu ambayo ni qumm.
 
Na Kar-balaa kwa Mashia ni bora kulikko Alqaaba. Imekuja katika kitabu(Bihaarul-anwar)kutoka kwa Abii Abdillah kwamba kasema;
"Hakika Mwenyezi mungu aliiteremshia Alqaaba wahyi (ufunuo) lau kama si udongo wa Kar-balaa nisingelikufanya bora ,na lau kama si mwili wa yule aliyeko katika udongo wa Kar-balaa nisingekuumba,wala nisingeumba nyumba ambayo kwayo umejifakharisha,basi tulia na uwe ni Mkia dhalili na si mwenye kibri kwa ardhi ya kar-balaa,la sivyo nitakutupa katika Jahannam" (Rejea kitabu Albihaar 10/107).

Bali Mashia/Rawafidhwah wanaona kuzuru kaburi la Husein huko karbalaa ni bora kuliko nguzo ya tano ya uislamu(Hijja)!!. Amesema Almajlisykatika kitabu chake (Bihaarul-anwar)Kutoka kwa bashiir addahaan amesema;"Nilimuuliza Abuu Abdillah(a.s) Endapo itanipita hijja alafunikaenda katika kaburi ya Husein? Akasema:Vizuri sana ewe Bashir,muumini yeyote atakae liendea kaburi la Husein hali ya kutambuahaki yake,katika siku ambayo sio siku ya idd,basi huandikiwa thawabu za Hijja 20 na Umra20 zenye kukubaliwa,na thawabu za kushiriki katika vita 20 vya Jihadi pamoja na Mtume au Imamu muadilifu, na atakaye liendea siku ya Arafa hali ya kujua haki zake basi huandikiwa thawabu zaHijja 1000 na Umra 1000 zenye kukubaliwa,na thawabu za kupigana Jihadi 1000 pamoja na Mtume au Imamu muadilifu.

Hivyo ndugu katika Imaan, mnawezakuona ni jinsi gani Mashia/Rawaafidhwah wanavyomtukuza la Hussein mjukuu wa Mtume (rehma na Amani ziwe juu yake) na Karbalaa ambapo ndipo alipouawa kwa dhulma kiasi cha kufifisha Arafa, Hijja kwa ujumla na Al Kaaba yenyewe. Si ajabu tena kuwaona vijana wao wakijipiga kwa minyororo na kuvuja damu wakiamini kuwa wanapaswa kujiadhibu hapa hapap duniani kwa kushindwa kumnusuru Al Hussein siku ile aliyouawa.

Haya tunayaleta huku tukijua kuwa kuna miito ya Umoja na Mshikamano wa Waislamu pasina hata kujali tofauti za kiaqeedah baina yetu. Miito hii ingawa ina lengo zuri lakini kupitia kushikamana huku hata na watu wa baatwili, aqeedah sahihi ya Ahlu Sunnah wal Jamaa inatoweka na sote tunajikuta tukiuvaa Ushia pasina kujua. Baada ya haya tunataraji wale wenye chembe chembe za Ushia watakuja juu labda waogope kujidhihirisha. Kwa wengi haya yanawezakuwa hayana uzito wowote kwani kwa zama za leo ambapo ujaahili wa kutokujua dini umedhihiri na kuweka mbele mas'lahi ya dunia, suala la aqeedah sahihi si jambo muhimu kwao. Tumeleta haya ili iwe kama alivyosema Allwah (Subhaanahuu wa taala);- "Ili aangamie mwenye kuangamia kutokamana na bayana na ahuike mwenye kuhuika kutokamana na bayana" (8"42). Aaangamie kiimani naahuike kiimani.

TUJIEPUSHE NA ITIKADI ZA KISHIA KATIKA MWEZI WA MUHARRAM TUSIJE KUANGAMIA.
Allwah ndiye Mjuuzi zaidi,

Ndugu yenu katika imaani,

Muhammad Issa