Saturday, November 17, 2012

MUHARRAM NA MASHIA

 Imebandikwa hapa leo hii 17/11/2012.
 
Assalaam alaykum.
 
Umekurubia kuingia mwezi wa Muharram, miongoni mwa miezi mitakatifu katika Uislamu iliyofuatana ambayo ni miwili kabla ya huo ujao (Dhul Qaadah na Dhul Hajji) na kisha mwezi wa Rajab. Katika mwezi huu wa Muharram, Mashia au Rawaafidhwah hufanya sherehe zao za masiku kumi ya Muharram ziitwazo Sherehe Ashuura.
 
Mashia wanaitwa pia Rawaafidhwah kwani jina hili kalitaja mmoja wa ma-Sheikh wao Almajlisy katika kitabu chake (Bihaarul-anwar) akasema katika mlango aliouita, mlango kuhusu ( Ubora wa raafidhwa na uzuri wa kujiita jina hili), kisha akataja kutoka kwa Sulaiman Al-aamash kuwa amesema: niliingia kwa Abii Abdillah Jaafar bin Muhammad nikasema kumwambia: Hakika watu wanatuita Raafidhwa, nini maana ya Raafidhwa? Akasema: wallwahi sio wao waliokuiteni hivyo bali Mwenyezi Mungu alikuiteni hivyo katika Taurati na Injili kupitia ulimi wa nabii Mussa na nabii Issa.( Tazama kitabu (Bihaarul-anwar) cha Almajlisy 65/97. (ambacho ni miongoni mwa marejeo yao muhimu katika vitabu vyao vya sasa)
Na imesemekana kuwa: wameitwa raafidhwa kwa sababu walikuja kwa Ally bin Hassan wakamwambia: Jitenge na Abubakari na Omar ili tuwe pamoja nawe, akasema: wao ni vipenzi wa Babu yangu, siwezi kujitenga nao bali niko pamoja nao, wakasema: hivyo basi tumekukataa, ndipo wakaitwa Raafidhwa, na akaitwa kila aliyemuunga mkono Zaid kuwa ni Zaydiyya.(Rejea: Attaaliqaat alaa matni lum-atul iitqaad cha Sheikh Abdallah Aljibriin uk.108).

Na inasemekana:wameitwa Raafidhwa kwa kupinga kwao utawala wa Abubakari na Omar (Radhi za Allwah ziwe juu yao) -Tazama Maqaalaatul-Islaamiyiin cha muhyiddiin Abdulhamiid (1/89) na imesemekana: Wameitwa hivyo kwa kukataa kwao Dini. (Tazama Ibid 1/89)
Kwa hiyo Mashia au Rawaafidhwah ni pote jengine kabisa mbali na Ahlu Sunnah wal Jamaa lakini waislamu wengi wanaojinasibu na Ahlu Sunnah wal Jamaa wamekumbwa na itikadi za Kishia na miongoni mwa hizo ni sherehe zao za Ashuura katika mwezi huu wa Muharram ambapo hukumbuka kifo cha Al Hussein Ibn Ali (Radhi za Allwah ziwe juu yake na Baba yake pia). Shubha inayopataikana hapa ni kwamba siku ya Ashuura imethibiti kwa hadithi za Mtume (Rehma na Amani ziwe Juu lake) alopofika Madinnah ana kuwakuta Mayahudi wakiadhimisha siku hii ambayo ni terehe 10 Muharram. Akawauliza ni siku gani hii mnayoiadhimisha? Wakasema ni siku Allwah alipomuokoa Musa na watu wake dhidi ya Firauni. Mtume akawaambia sisi ndio bora kwa Musa kuliko nyie. Hapo Mtume (rehema na amani ziwe juu yake) akamuarisha swahaba awatangazie watu kuwa yeye atafunga swaumu siku hiyo na iliyo kabla yake yaani "Yawmu Taasu'a". 
“Ashura”: Hii ni ile siku ya mwezi kumi Muharram (Mfunguo nne) na “Taasuaa”: Hii ni siku ya mwezi tisa Muharram. Dalili na ushahidi wa usuna wa kuzifunga siku mbili hizi ni ile hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Abbas-Allah awawiye radhi-“Kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alifunga siku ya Ashura na akaamrisha watu kufunga”. Bukhaariy [1900] & Muslim [1130]-Allah awarehemu.

Kwa hiyo kilicho Sunnah ni kufunga siku ya tarehe 9 na 10 Muharram kama alivyofanya Mtume (Rehma na amnai za Allwah ziwe juu yake) kinyume na wafanyavyo Mashia/Rawaafidhwah wafanyavyo kwa kuzifanya siku hizi za vilio na kujipiga miili hadi kutoka damu eti kwa kukumbuka kuuwawa kwa al Hussein Ibn Ali (Radhi za Allwah ziwe juu yake na baba yake Ali Ibn Abi Twaalib).
Itikadi za Mashia kuhusu kuuwawa al Hussein ibn Ali (ambazo ndiyo chimbuko la Sherehe zao za Ashuura/Muharram) zimewafikisha hata kukufuru juu ya Allwah na matukufu yake. Kwa mfano, Mashia wanaitakidi sehemu yalipo makaburi ya watu waliodai kuwa ni maimamu wao, au ambao ni maimamu kweli, kwa sehemu hizo ni sehemu takatifu,hivyo Alkuufa ni haram(sehemu takatifu),pia Karbalaa ni haram,na Qumm nayo ni haram. Na wanayo riwaya wanayo dai kuwa imepokelewa kwa Asswaadiq kwamba, Mwenyezi mungu anayo haram yake ambayo ni makka,na Mtume wake anayo haram yake ambayo ni Madina,na amiiril-mu`uminiina anayo haram yake ambayo ni Alkuufa,na sisi tunayo haram yetu ambayo ni qumm.
 
Na Kar-balaa kwa Mashia ni bora kulikko Alqaaba. Imekuja katika kitabu(Bihaarul-anwar)kutoka kwa Abii Abdillah kwamba kasema;
"Hakika Mwenyezi mungu aliiteremshia Alqaaba wahyi (ufunuo) lau kama si udongo wa Kar-balaa nisingelikufanya bora ,na lau kama si mwili wa yule aliyeko katika udongo wa Kar-balaa nisingekuumba,wala nisingeumba nyumba ambayo kwayo umejifakharisha,basi tulia na uwe ni Mkia dhalili na si mwenye kibri kwa ardhi ya kar-balaa,la sivyo nitakutupa katika Jahannam" (Rejea kitabu Albihaar 10/107).

Bali Mashia/Rawafidhwah wanaona kuzuru kaburi la Husein huko karbalaa ni bora kuliko nguzo ya tano ya uislamu(Hijja)!!. Amesema Almajlisykatika kitabu chake (Bihaarul-anwar)Kutoka kwa bashiir addahaan amesema;"Nilimuuliza Abuu Abdillah(a.s) Endapo itanipita hijja alafunikaenda katika kaburi ya Husein? Akasema:Vizuri sana ewe Bashir,muumini yeyote atakae liendea kaburi la Husein hali ya kutambuahaki yake,katika siku ambayo sio siku ya idd,basi huandikiwa thawabu za Hijja 20 na Umra20 zenye kukubaliwa,na thawabu za kushiriki katika vita 20 vya Jihadi pamoja na Mtume au Imamu muadilifu, na atakaye liendea siku ya Arafa hali ya kujua haki zake basi huandikiwa thawabu zaHijja 1000 na Umra 1000 zenye kukubaliwa,na thawabu za kupigana Jihadi 1000 pamoja na Mtume au Imamu muadilifu.

Hivyo ndugu katika Imaan, mnawezakuona ni jinsi gani Mashia/Rawaafidhwah wanavyomtukuza la Hussein mjukuu wa Mtume (rehma na Amani ziwe juu yake) na Karbalaa ambapo ndipo alipouawa kwa dhulma kiasi cha kufifisha Arafa, Hijja kwa ujumla na Al Kaaba yenyewe. Si ajabu tena kuwaona vijana wao wakijipiga kwa minyororo na kuvuja damu wakiamini kuwa wanapaswa kujiadhibu hapa hapap duniani kwa kushindwa kumnusuru Al Hussein siku ile aliyouawa.

Haya tunayaleta huku tukijua kuwa kuna miito ya Umoja na Mshikamano wa Waislamu pasina hata kujali tofauti za kiaqeedah baina yetu. Miito hii ingawa ina lengo zuri lakini kupitia kushikamana huku hata na watu wa baatwili, aqeedah sahihi ya Ahlu Sunnah wal Jamaa inatoweka na sote tunajikuta tukiuvaa Ushia pasina kujua. Baada ya haya tunataraji wale wenye chembe chembe za Ushia watakuja juu labda waogope kujidhihirisha. Kwa wengi haya yanawezakuwa hayana uzito wowote kwani kwa zama za leo ambapo ujaahili wa kutokujua dini umedhihiri na kuweka mbele mas'lahi ya dunia, suala la aqeedah sahihi si jambo muhimu kwao. Tumeleta haya ili iwe kama alivyosema Allwah (Subhaanahuu wa taala);- "Ili aangamie mwenye kuangamia kutokamana na bayana na ahuike mwenye kuhuika kutokamana na bayana" (8"42). Aaangamie kiimani naahuike kiimani.

TUJIEPUSHE NA ITIKADI ZA KISHIA KATIKA MWEZI WA MUHARRAM TUSIJE KUANGAMIA.
Allwah ndiye Mjuuzi zaidi,

Ndugu yenu katika imaani,

Muhammad Issa

No comments:

Post a Comment