Sunday, March 29, 2009

TOFAUTI KATIKA VIUMBE WA MWENYEZIMUNGU

Imechangiwa na Dada Saada al-Ghafry.

Kuna waganga wa kitabu wa kweli na matapeli, lakini kwa Tanzania wengi wao ni matapeli. Mganga akishakwambia "umefanyiwa hivi na xyz ", mara nyingi huyo xyz akiwa ni mpenzi wa aina moja ama nyingine kama ni kwenye familia au urafiki, ujue huyo ni tapeli. Kimbia haraka sana. Yapo matibabu ya Kitabu, lakini ni wachache sana wenye ujuzi huo, na tiba hiyo haistahili kupokea malipo.
Majini yapo, na ni kweli yapo mazuri na mabaya, kama walivyo wanadamu wazuri na wabaya. Vitendo vyema (vinavyotekeza amri za Mwenyeezi Mungu) vinamfanya jini na binaadamu wajulikane kuwa ni wazuri na wale wenye vitendo vibaya (vinavyoasi amri za Mwenyeezi Mungu) vinamfanya jini na binaadamu wajulikane kuwa wabaya. Sote ni viumbe wa Mwenyeezi Mungu kama walivyo wanyama na Malaika pia kuwa ni viumbe wa Mwenyeezi Mungu. Sote tumeumbwa ili tumuabudu Mwenyeezi Mungu. Binadamu na wanyama tunaonekana, Malaika na majini hawaonekani nasi ila kwa wenye elimu ya majini km Nabii Daud aliweza kuwafuga na kuwatuma majini. Wapo pia hivi sasa wenye elimu ya kufuga na kuwatumikisha majini, lakini Mwenyeezi Mungu amekataza shughuli hiyo. Nabii Daud alipewa ruhusa maalum, wengine hawaa ruhusa hiyo.
Kwa Kiarabu anaitwa jinn, na kwa Kiinglish anaitwa genie.

No comments:

Post a Comment