Sunday, March 29, 2009

HARAMU YA KUTABIRI KATIKA UISLAM

Imechangiwa na Bi Saada al-Ghafry.

Utabiri kwenye Uislam ni haram. Hakuna iitiradhi katika hilo. "Ilm alghaaib" ni ya Mwenyeezi Mungu peke yake. Haina mshirika.

Kuwa na elimu kuliko wengine ni neema kutoka kwa Mwenyeezi Mungu. Kuitumia vibaya (kwa kwenda kinyume ya maamrisho yake) ni dhambi. Ndiyo utakuta daktari anakwambia mgonjwa ana saa/siku/miezi/miaka kadhaa ya kuishi. Mwenyeezi Mungu anamuumbua. Anakufa daktari na mgonjwa anapona. Cha kusema ni kuwa sisi tunafanya kilicho kwenye uwezo wetu, yaliyobaki tunamwachia mwenye milki ya uhai na mauti.

Zoezi la unajimu, kwa watendaji na wafuasi, ni ushirikina kwenye Uislamu. Yahya Kufanya utabiri hakuhalalishi alichoharamisha Mwenyeezi Mungu, kama vile mapadre kulawiti watoto ni haram. Liwati haihalalishwi kwa vile mapdre wanafanya hivyo.

Ni mengi yaliyoharamishwa lakini yanafanywa. Ni lazima turudi kwenye vitabu na sio kuwatazama au kuwasikiliza wanaodai kuwa ni wafuasi wa vitabu.

No comments:

Post a Comment