Wednesday, March 11, 2015

KIPEPERUSHI [BROCHURE] CHA AHLUS SUNNA WAL JAMAA HAJJ & UMRA TRUST - TANZANIA

Ahlus Sunna Wal Jamaa Hajj & Umra Trust
Saba General Bldg. [Inatazamana na Anatouglou, Mnazi Mmoja]
Lumumba Street
DAR ES SALAAM

Simu: 0717 224437; 0785 972626; 0682 677259 au
Wanamume:  0765 462022; 9784 863539; 0713 298114
Wanawake:   0715 273306; 0754 436351; 0715 348009

Madrasat Ruhina
Rahaleo [Nyuma ya Jengo la Radio, Zanzibar
ZANZIBAR: 

Simu:  Wanamume:  0657 606708; 0777 458075;  0685 366141
           Wanawake:   0777 426053; 0777 499918; 0777 428340

Mr. Khalfan Kabbuu [Kidishi]
Macho Manne Traders,
Chake Chake
PEMBA

Simu:  0777 497300; 0773 222542; 0776 357117; 
           0777513627; 0777429415; 0778682071

Akaunti za Benki:
AHLUS SUNNA WALA JAMAA HAJJ AND UMRA  TRUST
1.  Amana bank Tshs.:  001120024610001
                          USD: 001120024610002

2. PBZ  Bank  Tshs.:  51120100001378
                        USD: 51120200001383

3.  CRDB Bank: Tshs.:  01J1024740300
                           USD:  02J1024740300

Ukurasa  wa 2

AHLUS  SUNNA  WAL JAMAA 
Tunasimamisha  nguzo ya Hijja kuendeleza Uislam

 Hadith


"DINI NI NASAHA"

Soma Unasihike

Tuko karibu, tunasali sala 5 katika Misikiti Mitakatifu
GHARAMA ZOTE NI DOLA  (USA) 4,500.

Ukurasa wa 3
1.  KAMILISHA NGUZO ZA DINI YAKO !
Ewe Muislam,  HIJJA NI NGUZO KATIKA UISLAMU,  mwenye kuisimamisha amesimamisha Dini.  Thibitisha  Uislamu wako kwa vitendo upate Radhi za moja wako!  Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako na kuanza kufaidi matunda ya Hajj.  Karibuni Ahlus Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora.  

2.  HIJJI, UFE  MUISLAMU
Mtume [SAW]  amesema kuwa anayekufa bila kuhiji hali ya kuwa aliwahi kupata uwezo anakufa Yahudi au Nasara, na Uislam hautomtambua!  Hijja ni haki ya Moja wako iliyopo juu yako!  Mpe Mola wako haki yake kwanza kabla ya kufanya mengine.  

3.  HIJJI UDHAMINIWE NA ALLAH!
Mtume [SAW] amesema kuwa Mwenye kuhiji amedhaminiwa na ni mgeni wa Allah.  Tupende sana kwenda kuwa wageni wa Mwenyezi Mungu  na kuyaweka maisha yetu katika udhamini (bima) ya Mola Mkarimu.  Tulishaitwa sote tangu zama za Nabii Ibrahi (AS), na hakuna wito mwingine binafsi.  

4. JEE, UMESHAMZURU MTUME WAKO?
Mtume [SAW]  amesema  "Mwenye kuja kunizuru baada ya mauti yangu ni kama aliyenitembelea wakati wa uhai wangu".  Neema iliyoje kumzuru Mtume [SAW] !  Na huu ni ushahidi wa imani na mapenzi ya muislam.  Wewe umeshamzuru  Mtume [SAW] mara ngapi?  Yako wapi mapenzi yako kama hujamzuru Mtume wako? Karibuni wapenzi wa Mtume [SAW]!

5.  TAJIRIKA  KWA  KUHIJI !
Mtume [SAW] amesema "...Mahujaji wanarudishiwa kila walihokitumia katika Hijja, shilingi moja kwa milioni moja."  Hivyo Hijja ni kitega uchumi bora kabisa.  Haweza kuwa fakiri abadan mwenye kutekelea Hijja!  Karibuni Ahlus Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora.


6.  MANUFAA  YA  HIJJA
Mtume [SAW]  anasema, "Mwenye kwenda kuhiji akifa safarini anatiwa Peponi.  Akirudi salama kwao anarudishwa na ujira mkubwa na zawadi nyingi".  Na akasema tena Mtume [SAW] "Husamehewa mwenye kuhiji na anaowaombea". Twendeni na kupeleka wengine kwa faida ya  Umma wa Waislam.

Ukurasa Na. 4

7.  AMKA,  MUISLAM  MTANZANIA !
Unajua kuwa Tanzania tuko nyuma sana katika utekelezaji wa nguzo ya Hijja?  Tunakwenda wachache sana, na wengine wetu tukiwa wazee tumeshachoka.  Mtume [SAW] amehimiza  watu waende Hijja wakiwa vijana wenye nguvu.  Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako na uboreshe maisha yako kwa udhamini wa Moja wako.  

8.  KILA ENEO LIPELEKE MAHUJAJI
Qur'ani imedhamini kuwa tutakwenda Hijja kutoka milima na mabonde ya mbali {Al-Hajj: 27}.  Yaani Mwenyezi Mungu [SW] tutoke kila Mkoa, Wilaya, na Mtaa kwenda Hijja kila mwaka.  Kila siku tunamuomba Mwenyezi Mungu aboreshe maisha yetu.  Lakini sharti lake Allah anataka tuitikie Wito Wake kwanza ! {Al-Baqara:  186} Je? tunaitika?

9.  UOMBEZI WA MTUME [SAW]
Mtume [SAW] amesema "Mwenye kuja kunizuru mimi kwa kutaraji ujira kwa Allah, basi mimi nitakuwa muombezi na shahidi wake (siku ya Kiyama)".  Neema iliyoje kupata fursa kama hii!  Sote tunauhitaji uombezi huu.  Wahi sasa kuja kulipa uitakase  mali yako na kujihakikishia uombezi wa Mtume wako [SAW].  Karibuni wapenzi wa Mtume [SAW] !

10. HASARA  ZA KUTOHIJI NI KWETU SOTE !
Allah anasema tuitangaze na kuhimizana kwenda Hijja (Al-Hajj: 27).  Kwasababu baadhi yetu wana uwezo na hawaendi  Hijja Mwenyezimungu amesema kwa hasira, "Hana haja na viumbe sote" (Aal-Imran: 97).  Hivyo, hasara ni yetu sote! Karibuni Ahlus Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora.

Ukurasa wa 5

11.  "AL-HAJJ"  NI  KIPENZI  CHA ALLAH !
Katika Ala na Vitakatifu vya Allah ambavyo Ameonya visivunjiwe heshima, bali vitkuzwe kwa faida ya muumin, vingi sana vinapatikana Makka na Madina (Al-Maaidah: 2, Aal-Imran: 96).  Umeshaziona alama zake Allah na kujikurubisha kwa Mola wako?  Makafiri wanaichukia sana Hijja; kwa hivyo Waislamu tuipende sana!.

12.  MTUME ANAHIMIZA !
Mtume [SAW] ameagiza, "Fanyeni haraka kwenda kuhiji!".  Tunahimizwa tuende kuhiji  tungali vijana ili maisha yetu yadhaminiwe na Allah.  Baada ya kupata uwezo, ni makosa kuakhirisha kwenda kuhiji.  Masahaba, vijana na wazee, walihiji Hijja nyingi sana.  Wewe je? Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako na kufaidi matunda ya Hijja.

13.  AFYA,  UWEZO  NA  NAFASI
Tunahitaji afya, uwezo, na nafasi ili kutekeleza Nguo ya Hijja.  Rasilimali hizi Ametupa Allah tuzitumie anavyotaka yeye!  Hakuna mwenye uhakika wa  kufika mwakani Mjuto mjukuu.  Unangoja nini? Usimwendekeze shetani (ibilisi).  Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako na uboreshe maisha yako kwa udhamini wa Mola wako.  

14.  WAOKOE  WAZAZI WAKO!
Masahaba waliwahijia wazee wao waliokufa bila kuhiji na waliokutwa  wamezeeka ilipofaradhishwa Hijja.  Hivi sasa waislamu wengine wanakufa bila kuhiji na kuacha mali zaidi ya malipo ya Hijja.  Hivyo walikuwa na uwezo wa kuhiji!  Uislam hauwatambui wazee hao mpaka wahijiwe!  Umeshawaokoa wazazi wako na kuwarudhsia katika Uislamu?

15.  MATAJIRI  WA  KIISLAMU !
Mtume [SAW] amesema "Kutoa katika Hijja ni sawa na kutoa katika Jihadi, shilingi moja kwa mia saba".  Uwezo wa baadhi yetu ni uwezo wetu.  Waislamu ni kama jengo au kiwiliwili kimoja.  Tupelekane Hijja na tusaidiane kuisimamisha nguzo ya Hijja! Kadiri tunavyokwenda wengi Hijja, ndivyo Allah atavyotupa utukufu na nguvu nchini mwetu.  

16.  TUSHIRIKIANE KUPELEKANA HIJJA !
Wajibu wa kwenda Hijja unawahususu mwenye uwezo na WENYE UWEZO (Aal-Imran: 97).  Inawezekana, kwa kuchanga, tukapelekana mmoja mmoja Hijja kila mwaka katika familia, mtaa, msikiti, na kadhalika.  Bila shaka  Allah atalifurahia hili na atamimina neema kuwa juu yetu.  Tuchangishane katika kheri kwa faida yetu sote, Waislamu, tusisubiri, tuchukuwe hatua !

Ukurasa wa 6

17.  WAPI  KAMA "ARAFA"?
Hijja ni kama Kutano Mkuu wa wailamu wote duniani.  Allah anatukusanya sote katika bonde la Arafa ili tujuane na tumiminie Radhi Zake na kuyabariki maisha yetu.  Kila mmoja wetu anatakiwa afike hapo angalau mara joja katika umri wake, na ajsikie ndani ya moyo wake kuwa yu miongoni mwa waislamu.  Ndugu yetu, wewe umeshahudhuria hapo mara ngapi?

18.  KUPATA PEPO KWA SIKU TANO !
Hakuna kitu kinachowalia wenye akili aidi kuliko vipi kuokoka na Moto na kupata Pepo!  Hijja peke yake ndiyo inayoweza kumsafisha muislamu na madhambi yote, na akapata Pepo katika muda wa siku tano.  Hivyo, hakuna matumizi bora ya fedha, nguvu na nafasi ya mja kuliko kwenda Hijja.  Wewe ndugu yetu ushakwenda mara ngapi?

19.  HIJJA INAZAA  UMOJA NA NGUVU
Hijja inawakusanya waislamu toka kila pembe ya dunia bila kubagua kabila, taifa, wala akida.  Hijja ni zoezi na fundisho kubwa la umoja wa waislamu. Allah anatuita huko tukapate manufaa Aliotuandalia (Al-Hajj: 27).  Utukufu, nguvu na ushindi ni vya Allah!  Twende wengi kutoka kila pembe ya nchi yetu tukapate nguvu zitokazo kwa Allah.!

20. UMESHAWAPELEKA  WATOTO  HIJJA?
Sahaba mmoja alimnyanyua mtoto wake mdogo na kumuuuliza Mtume [SAW], "Na huyu ananufaika na Hijja?"  Mtume [SAW] akajibu "Ndio, na wewe unapata ujira"  Wangapi tumewapeleka watoto wetu Hijja?  Milioni ngapi tunwatumilia kwa mambo ya fahari?  Karibu uwaandikishe watoto na wafanyakazi wako.  Karibuni Ahlus Sunna Wal Jamaa, kwa mipango mizuri, huduma bora na uongozi mzuri wa ibada.

GHARAMA ZOTE NI DOLA  4,500

Sheikh Muhammad Dedes
Simu:  0655 462022;  0682 462022; 0777 462022.
Email: muhammad.dedes@yahoo.com


Mwisho  wa Kipeperushi

NYIRADI  ZA  ARAFA  BAADA YA  KUSWALI  DHUHR/LAASIR KUELEKEA  QIBLA  

BISMILLAHI RAHMAANI  RAHIIM
Labayka Allahhumma Labayka
Labayka Laa  sharika  Laka Labaika
Inna l-hamda, Wanni-mata,  Laka walmulk
Laa Sharikika Laka x 3

Laailahailla lahu wahdahu Laa sharikalah
Lahulmulku walahul hamdu yuhyii wayumiitu
Biyaidihi ikhairu wahuwa alaa kulli shai-in Qadiir x  100

Laahaula walaa quwwata illa billahi l-aliyi l-adhym.
Ashhadu annallaha alaa kulli shain qadiiru
Wa annalaaha qad-ahaatwa bikulli shain - ilmaa x 100

Audhu billahi mina  sshaitwaani rrajiim
 inna llaha huwa  ssamiyul-aliim x 3

Kisha SOMA ALHAMDU MPAKA MWISHO  x 3
Kisha QULHU WALLAHU AHADU MPAKA MWISHO x 3
Kisha
BISMILLAHI RRAHMAANI  RAHIIM
ALLAHUMA SWALI ALLA NNABIYYI L-UMMIYI  WARAHMATULLAHI  WABAKATUH x 100.




M U O M B E     M O L A      MTUKUFU   M A M B O   Y O T E   U T A K A Y O.






No comments:

Post a Comment