Sunday, July 22, 2012

WARAKA MAALUM WA WAWAKRISTO ZANZIBAR - TOKA 2009!!!

Umoja wa Wazalendo Zanzibar June 24, 2009 WARAKA MAALUM KWA WAKRISTO ZANZIBAR Wapendwa katika Bwana Ndugu Wakristo umefika wakati tumeonelea kuwa ipo haja ya kuwaelezeni machache ili kuona maendeleo yetu na mafanikio tuliokwisha yapata hapa Zanzibar, yanaendelezwa na hayarudi nyuma kwa namna yoyote. Hapana shaka kuwa munaelewa kuwa idadi yetu hadi sasa bado ni ndogo sana na wengi wetu tungali katika kiwango na hadhi ya wahamiaji na sio Wazanzibari kama wanavyosema wenyewe. MAFANIKIO YETU Kabla kugusia yale ambayo tunahisi ndio lengo la waraka huu hapana budi kuwatajieni mambo machache ambayo tumefanikiwa kuyapata hadi sasa. Pamoja na jitihada zetu za muda mrefu bado tunapaswa tumsifu Bwana kwa msaada wake mkubwa kwetu dhidi ya maadui zetu. Tunaamini kuwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, Bwana atatupa ushindi na mafanikio makuu zaidi ya haya na atawafumba macho maadui zetu wazidi kulala ili mipango yetu yote ya kuibadilisha Zanzibar kidemografia ifanikiwe katika kipindi kifupi kijacho. Mafanikio yetu yameenea katika kila upande - katika uchumi, siasa, huduma za serikali, umiliki wa ardhi, ujenzi, elimu, n.k. Ili kupata picha kamili ni vyema tuorodheshe kwa ufupi mafanikio hayo: 1. Nafasi yetu kwa upande wa elimu imekua ya kuridhisha kupitia nafasi za serikali. Hivi sasa ni rahisi na limekua jambo la kawaida katika kila matangazo ya wito wa masomo kusikia majina ya Wakristo. Kati ya vijana saba hadi kumi, ni lazima upate vijana wawili hadi watatu kutoka katika makanisa yetu. 2. Sambamba na matangazo ya elimu vijana wetu wamekuwa wanapata nafasi nyingi za ajira katika Serikali ya Zanzibar. Hali ya kutoelewana kisiasa baina ya Wazanzibari imetoa mwanya kwetu kuingiza vijana wa Kikristo wenye asili ya bara kwa wingi kwani wamekuwa wanaaminika zaidi kuliko vijana wa Zanzibar. 3. Hali tulioieleza juu imetuwezesha pia kuwa na Wakristo wengi katika nafasi za juu serikalini na katika chama tawala. Hali hii ni lazima iendelezwe katika ngazi zote kwani imekuwa ikitusaidia hasa katika kiwango cha masheha na kamati zao kwani huku ndiko kunako mambo mengi ya kila siku. 4. Tumepata fursa ya kutumia Taasisi za serikali kwa uendeshaji wa ibada zetu hali hii imefanya tuzidi kukubaliwa na Waislamu na kuvumiliwa na inaweza kutupa nafasi ya kuwavuta katika NENO LA BWANA. 5. Kwa upande wa mashamba (vijijini) tumepata wasaa mzuri wa kununua ardhi toka kwa Waislamu ambao hadi sasa bado hawajashtuka. Ardhi hizi zimetuwezesha kujenga makanisa kadhaa ambayo hapo awali hayakuwepo. 6. Idadi ya skuli na vituo vyetu (ambavyo licha ya picha ya juu kuwa haviendeshwi kwa misingi ya Kikristo lakini kiukweli ni vituo vya kimisionari) vimeongezeka kwa hali ya kuridhisha. Skuli hizi nikuanzia kwa watoto wadogo hadi vituo kama hichi kilichopo Mji Mkongwe (Stone Town Youth Centre) na zinafanya kazi vizuri katika kupandikiza mila za Kikristo. 7. Sera ziliopo hivi sasa kwa upande wa uingiaji na utokaji Zanzibar imetusaidia sana katika uingiaji wetu (Wakristo) kutoka Bara na hivyo kusaidia kufuta ile imani ya kuwa Zanzibar ni kisiwa cha Waislamu na eti Wazanzibari kwa zaidi ya aslimia 99 ni Waislamu. 8. Ujaji wa Wakristo kwa wingi kutoka bara kwa kazi za kiserikali na Chama umewezesha kuongezeka kwa idadi ya mabaa na klabu za pombe kuwahudumia. Hivi sasa ni jambo la kawaida kuona magari ya aina mbalimbali yanayomilikiwa na eti Waislamu yanabeba kreti za pombe kali. 9. Kujiingiza kwetu katika Taasisi za dola katika ngazi za mitaa kumetuwezesha kupata nafasi ya kutangaza Ukristo kwa njia ya mihadhara ya Injili. 10. Tumefanikiwa kupata viwanja vingi katika maeneo ya Mjini ambayo yangali mapya. Maeneo haya ni kama Tomondo, Mombasa, Mwanakwerekwe, n.k. ambayo tayari tumeshajenga makanisa yetu ingawaje kwa sasa hayajawa na waumini wengi wa kuyatumia na bado yanaonekana ni matupu. Ndugu wapendwa katika bwana, Mafanikio hayo yasitufanye tukalewa na kusahau jukumu la kanisa la kuona kuwa utawala wa Bwana unashuka Zanzibar haraka iwezekanavyo. Kosa lolote tutakalofanya hivi sasa litaweza kuturudisha hatua kadhaa na huenda nafasi hii tulionayo hivi sasa tusiipate kwa karne mpya ijayo. Mambo ya kufanya yanayotukabili ili kuimarisha nafasi yetu na kuona yale tuliokwisha yapata hayatutoki na kuyafanyia dira kwa karne ijayo ni haya yafuatayo: Tusahau tafauti zetu dhidi ya adui Ingawaje tupo madhehebu nyingi lakini tunawajibika kuelewa kuwa Waislamu na Uislamu wao ni adui yetu namba moja ambaye hatutofaulu kupambana nae mmoja mmoja. Uislamu hapa Zanzibar ni dini iliofungamana na mila na utamaduni hivyo kila itakapowezekana tusahau tafauti zetu ndogo ndogo na hata kubwa kukabiliana nao, vyenginevyo tutarudi kama wakati wa Karume. Tuhakikishe tunapata ardhi Hii ni mbinu kongwe katika usambazaji wa Ukristo. Wazee wetu walipoleta Ukristo Zanzibar na katika Afrika jitihada waliyofanya ni kupata ardhi kubwa kwa ajili ya ujenzi wa maeneo yetu majengo ya hospitali, shule, zahanati, vituo vya chekechea, makanisa n.k. Tunahitaji ardhi kubwa ili kuziweka huduma hizo mahala pamoja kwa ajili ya kueneza injili ya bwana na Muokozi wetu. Tununue nyumba na viwanja kwa ujenzi wa makanisa Inaonesha Waislamu wenye siasa kali na baadhi ya watendaji kwenye sirikali wameanza kushtuka na ongezeko kubwa la makanisa katika kisiwa cha Unguja. Kuna dalili kuwa tunaweza kupata ugumu katika kupata viwanja kwa ajili ya makanisa. Njia tunayoweza kuitumia kwa muda huu ni kununuwa viwanja vitupu au nyumba za Waislamu kwa bei kubwa itayowashawishi kuviuza na baadae tutaweza kuvijenga au kugeuza nyumba hizo kuwa makanisa. Tujenga shule na hospitali kwa wingi Hizi ni taasisi pekee ambazo tunaweza kuzitumia kueneza neno la Bwana kwa Waislamu walio wengi hapa Zanzibar. Kwa kutumia umasikini unaowakabili wengi ya Wazanzibari na uchache wa huduma hizo tunaweza kujitangaza vizuri, tujitahidi kutoa huduma nzuri kuweka vifaa vya kisasa kuweka bei ndogo kuweka upendo ili vituo vya Waislamu au hata vile vya serikali visiweze kuvikaribia vyetu. Shule ni sehemu muhimu ya kupandikiza mafundisho yetu, zaidi kwa watoto wadogo (Nursery). Tunadai muda zaidi katika Vyombo vya habari (Tv na Redio) Kwa muda mrefu sasa uislamu na waislamu wamehodhi vombo hivi vya habari mbali na kuwa siku ya ijumaa ambayo yote humilikiwa na vipindi vya kiislamu vyombo hivyo hutenga siku nyengine kadhaa kwa vipindi vya kiislamu na hata kuthubutu kutia adhana kila wakati wa sala hali hii inaudhi na inatoa picha ya wazi ya serikali kupendelea uislam ingawaje inadai kuwa haina dini. Wakati wa kusherehekea miaka 25 ya TVZ tulizungumzia suala hili lakini inaonekana halikupata mtu wa kulifanyia kazi. Sasa tuhakikishe kuwa ukristo unapata muda zaidi katika vyombo hivyo au uislam nao upunguziwe nafasi. Tuongeze mihadhara ya wazi Wakati Waislam wamezuiliwa kufanya mihadhara ya wazi, sisi tujitahidi kuhakikisha kuwa mihadhara yetu inaongezeka kwa kiwango kikubwa na inakuwa ya amani kupingana na ile ya kwao ya vurugu. Kwa kuwa Waislamu hawahudhurii mihadhara hiyo, lazima tuone wakristo wa Mjini na Mashamba wanahamasishwa na kupatiwa nyenzo ili kuhudhuria. Vipaza sauti vitumike kuhakikisha kuwa neno la bwana linafika kila pahala. Mihadhara ifanyike karibu na nyumba, misikiti na kwenye viwanja vya wazi. Tuendelee kutumia shule na sehemu za Umma Ili kuwafanya waislamu watuzoee na kuondosha chuki yao kwetu ni lazima kuendelea kutumia mashule na sehemu za Umma zilizo wazi kwa mambo yetu ya ibada kwa kipindi kirefu hali hii inaweza kuwafanya washindwe kuona tafauti kati yetu na wao na hivyo kutuzoea haswa watoto wao. Tufanye suala la uhamiaji Zanzibar kuwa jepesi Uzoefu unaonesha kuwa ni jambo gumu kuwabatiza Wazanzibari waislamu. Hali hii inafanya ongezeko la wakristo kuwa dogo au halipo kabisa ukitoa wale wanaozaliwa katika familia za kikristo. Njia pekee ya kuhakikisha ongezeko la makanisa na Taasisi zetu ni kuongezeka kwa wakristo. Jambo hili litawezekana kwa kuingiza Wakristo wengi kutoka Tanzania Bara au wapagani ambao tutaweza kuwabatiza kwa kutumia udugu wetu wa kikabila au asili ya Bara. Kwa kuwatumia ndugu zetu waliomo serikalini (SMZ au SMT) tuhakikishe kuwa suala la uhamiaji linabakia wazi na rahisi na linaendelea kwa kila hali. Tuzuie jaribio lolote la kadi za uraia au vitambulisho Wakristo tunapaswa kuelewa kuwa iwapo serikali ya Zanzibar itaamua kufanya cho chote ili kuwa na vitambulisho au kadi za uraia kwa wazanzibari pekee basi jambo hilo litaathiri sana mipango yetu ya muda mrefu kwa Zanzibar. Iwapo tutawajibika kuunga mkono ni kadi za Uraia na vitambulisho vya Watanzania kwa Ujumla na sio Zanzibar peke yake. Tujipenyeze Vyamani na kushika nafasi muhimu Lazima tuelewe kuwa chama cho chote cha siasa kinalenga kukamata serikali ili kiweze kutekeleza yale yanayoaminika kuwa ni mazuri kwa chama hicho. Tunapozungumzia vyama vya siasa kwa Zanzibar tunahusisha zaidi kwenye CCM na CUF. Watu wetu wamefaulu kuingia kwa wingi katika chama tawala na katika jumuia zake. Tupenyeze wenzetu serikalini Sambamba na suala tulilolielekeza juu, hatuna budi kusomesha vijana wetu na kuhakikisha kuwa tunatumia kila njia na ushawishi ili kuwaingiza serikalini na hasa katika sehemu muhimu. Hii itarahisisha kuungwa mkono mipango yetu na kupunguzwa vikwazo kwa mikakati yetu. Tuunge mkono sera za utalii Hadi sasa wengi wa watalii wanaoingia Zanzibar hutokea nchi za Kikristo. Desturi za watalii hupingana na zile za Kizanzibari na hata za Kiislamu. Watalii wanasaidia kuongezeka kwa mabaa na vivazi ambavyo waislamu wanataka visivaliwe hasa na wanawake. Tujenge mabaa na kuongeza pombe Waislamu wengi huchukia pombe na huweza kuhama iwapo duka la pombe au baa ipo karibu nao. Waislamu hatari ni wale wanaosoma na kupata muda wa kujishughulisha na dini yao. Pombe ni kitu ambacho humtoa Muislamu katika Uislamu wa vitendo na kumkaribisha na Ukristo. Tuwafuate Wakristo waliosilimu ili warudie Ukristo Watu wa aina hii wanakuwa bado hawajatulia na mara nyingi huwemo katika matatizo.. Pana haja ya kuwalenga watu hawa ili kuwarudisha kabla hawajatulia au kupata elimu nzuri. Matatizo yao ndipo mahala pa kuanzia ili Bwana awateremshie roho ya utulivu. Uzima wa Ukristo ni kuwa na wafuasi wengi kadiri iwezekanavyo. Tuwafuate wanawake kwa misaada Jumuiya zisizo za kiserikali zinaungwa mkono duniani kote na hasa zile za wanawake na watoto tujiweke pamoja ili tuweze kuwavutia wanawake kwa jina la kuwasaidia. Tuongeze vituo vya mafunzo ya kikristo Kituo cha vijana cha mji mkongwe (Stone Town Youth Centre) kimekuwa kikifanya kazi yake vizuri kwani hadi sasa lengo lake la ndani bali (bado) halijaeleweka na vijana wanaohudhuria hapo kwa shughuli mbali mbali, jitihada zifanyike ili kuwa na vituo vya aina hii katika maeneo mengine. Lengo kuu liwe ni vijana na wanawake bila ya kuonesha dalili za kidini. Tuwaowe wanawake wao kwa kusilimu kimajina Jitihada za makusudi zifanyike ili kila itakapowezekana kuwaoa wanawake wa Kiislamu ili tuweze kuwabatiza baadae, njia nzuri iwapo patakuwa na ugumu ni kusilimu kiuongo ili kuruhusiwa kuwaoa wanawake wao. Tuanzishe NGOS na sisi tuwe viongozi Kwa hivi sasa wafadhili wengi wameonesha hamu ya kuzisaidia NGO’s moja kwa moja badala ya serikali ni lazima tujitahidi kuunda jumuiya zetu ambazo zitawashirikisha waislam lakini uongozi wa juu ni lazima uwe mikononi mwetu. Hii itatuwezesha kuona sera zetu na malengo yetu yanatekelezwa kupitia kivuli hicho. Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti waislam Mambo yetu mengi yamekuwa yanakwenda vizuri katika maeneo mbali mbali baada ya wenzetu kuwemo katika kamati za masheha na matawi ya vyama na kamati za maendeleo za maeneo mbalimbali. Hali hii ni lazima iongezeke ili udhibiti wa shughuli za waislam uwe mzuri zaidi na wakati huo huo kuona kuwa mambo yetu yanakwenda yakiwa na baraka ya vyombo vya dola na vyama vya siasa. Tuwachonganishe mashehe wenye msimamo mkali Mashehe wenye msimamo mkali wamekuwa ni tatizo kwa ukristo kwani wana wafuwasi wengi na wamekuwa wakisema wazi na kushutumu maendeleo yetu. Mashehe hao ni lazima wachonganishwe na serikali ili hali ikiruhusu wazuiliwe kuendesha shughuli zao. Wakati tukifanya hivyo hatuna budi kuwaunga mkono mashehe wote ambo wamekuwa wakitusaidia kwa njia mbali mbali. Tulenge kuifuta tabligh Pamoja na kuwa tabligh sio hatari moja kwa moja kwa ukristo lakini bado inastahili kupigwa vita kwa sababu ni aina pekee ya mihadhara ya waislamu inayoruhusiwa humu Zanzibar. Tabligh inaweza kuwazindua baadhi ya waislam ambao ni vyema kubaki bila ya kuzinduliwa. Tulete waumini kutoka mashamba kuanza makanisa Hivi sasa pameibuka wasi wasi kuhusiana na wingi wa makanisa ambayo hayajapata waumini wa kuyajaza. Ili kuficha dosari hii na hoja kadhaa utaratibu uliopo hivi sasa chini ya baadhi ya makanisa ni lazima uungwe mkono. Wakristo wahamiaji wengi hufikia mashamba hivyo pawekwe na utaratibu wa kuwaleta mjini ili kujaza makanisa. NENO LA MWISHO Wapendwa katika Bwana. Miongozo hii ni mikubwa na inaweza kuwatisha baadhi ya waumini wa kikristo hasa wale ambao bado hawajampokea Roho Mtakatifu vizuri. Hata hivyo kwa uwezo wa Bwana Mungu wetu ni mpango rahisi. Suala la muhimu ni haya kufahamika na kila mkiristo apendae kumtumikia Bwana. Pia hatuna budi kuishukuru awamu ya nne ya serikali ya mapinduzi ambao imefungua milango kwa Ukristo na kushuhudia ongezeko la makanisa. Bwana awe nasi!

No comments:

Post a Comment