Wednesday, January 21, 2015

MAHAKAMA YA KADHI NDANI YA KATIBA PENDEKEZWA TANZANIA

MAHAKAMA YA KADHI

Written By Mohamed Said on Tuesday, January 20, 2015 | 10:22 AM


[07:00, 20/01/2015] Ally Abubakar:


Sheikh Hamid Jongo
1.       Leo kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 11 jioni tulikuwa ktk ukumbi Wa Julius Nyerere Conference  katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala tukiwawasilisha mapendekezo ya Muswada wa Mahakama ya Kadhi. Tulikuwa taasisi 11: Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Tanzania, Annahar, Basuta, Tampro, Dumt, Shura ya Maimamu, jumuiya na taasisi mbalimbali kwa upande mmoja na Bakwata upande wa pili, Tanganyika Legal Society (TLS) nk nk. Pia alialikwa Jaji Robert Makaramba na Arcado Ntagazwa.
2.      Maoni ya Jaji Robert Makaramba ni kuwa Mahakama ya Kadhi ni chombo halali na hakipaswi kuitwa cha kidini bali ni chombo cha dola, kigharamiwe na dola, Wakristo wasilalamike sababu hata mahakama za kawaida zinatumia sheria za Kikristo ambazo zinatokana na Common Law.  
3.      Bakwata wao wameiambia Kamati ya Bunge kuwa Mahakama ya Kadhi ni mahakama ya kidini hivyo isigharamiwe na dola bali zijigharamie zenyewe kama  tunavyogharamia ‘’maji ya udhu,’’ ‘’mikeka’’ na ‘’umeme,’’ misikitini, pia Mahakama ya Kadhi hiyo ndiyo hii Mufti aliyoiunda, na kwamba Mufti anayetajwa na muswada awe ni Mufti wa Bakwata hiyo iwe rasmi ndani ya sheria. Maoni ya Bakwata yamewasilishwa na Katibu wa Bakwata Mzee Lolila na Sheikh Hamid Jongo.
4.      TLS wao wanapendekeza muswada huu uondolewe haufai.
5.      Maoni yetu ya taasisi 11 kama yalivyoandaliwa na wanasheria kwa ushirikiano na masheikh yamewasilishwa na Wakili Njama. Kimsingi tumesema huu muswada haufai uondolewe na badala yake kamati tumeiomba ipokee muswada mbadala tuliouandaa ambao unaunda Mahakama ya Kadhi, unaunda Bodi ya Sheria za Kiislam ambayo ndiyo itakayoteua makadhi na kudhibiti nidhamu za makadhi, pia Waziri wa Sheria asipewe mamlaka ya kutunga sheria au kanuni zinazohusu Waislamu bila ya kushauriana na wanazuoni. Mahakama ya Kadhi tumetaka iwe sehemu ya “Judiciary,” igharamiwe na dola. Bakwata na Mufti wa Bakwata wasiwe ndiyo wateuzi wa makadhi. Tumeitaka Kamati ya Bunge iishauri serikali iuondoe muswada wake haufai na wala haukidhi vigezo vya kuunda chombo chenye hadhi ya mahakama. 
6.      Ntagazwa ameeleza historia ya Mahakama ya Kadhi na ameeleza kuwa muswada huu hauna nia ya dhati kuanzisha Mahakama ya Kadhi ya ukweli bali nia ni kupata kura za Waislamu tu. Ntagazwa aliungana nasi kuwa muswada uondolewe.
7.      TLS nao waliunga mkono hoja zetu kwa kiasi kikubwa. Katika kikao hicho kwa upande wetu tulikuwa mimi, Wakili Njama, Dr. Benhajj, Wakili Hamza Jabir, Masheikh: Kundecha, Kilemile, Sheikh Bawazir, Sheikh Mbalamwezi Mwanahistoria Mohamed Said na wengi wengine. Alhamdulillah tuliwakilisha vyema na wrote walituelewa tunaamini kazi tuliitimiza yaliyobaki Allah anajua zaidi. Mjadala ulikuwa mkali kutwa nzima lakini tuliwatuliza.
[07:00, 20/01/2015] Ally Abubakar: Aliandika makala Hii ni ndugu ktk Uislam, Mwanasheria/Wakili  Juma N. Dovutwa.

No comments:

Post a Comment