Tuesday, December 8, 2009

KUMWITA MWENYE ENZI MUNGU MAHAKAMANI NI KUMKUFURU

HABARI HII NIMEINUKUU KUTOKA GAZETI LA MWANA-HALISI LA TANZANIA LA Jumatano Disemba 2-8, 2009, ukurasa wa 9.

MUNGU AITWA MAHAKAMANI: Habari hii inasomeka kama ilivyo hapa chini:

MUNGU ameponea chupuchupu.
Jaji MARLON POLK wa Marekani ametupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa dhidi yake. (Astaghfirullah).

Jaji amechukua hatua hiyo kwa maelezo kuwa anuwani ya MUNGU haipatikani na hivyo hawezi kupeleka Samansi (summons) ya kutwa shaurini.

Kesi hiyo ya aina yake ilikuwa imefunguliwa na Seneta wa NEBRASKA, ERNIE CHAMBERS (pichani) ambaye sasa anasema anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Jaji.

CHAMBERS alitaka itolewe amri ya sitisho la VIFO, UHARIBIFU na UGAIDI "VINAVYOSABABISHWA NA MUNGU".

Jaji Polk alisema katika uamuzi wake kwamba mlalamikaji alipaswa kuwa na uwezo wa kumfikia Mshitakiwa ili kesi yake iweze kuendelea kusikilizwa.

"Kutokana na mahakama hii kugundua kuwa hakuna uwezekano wa samansi kumfikia mtajwa kwenye kesi husika, mahakama hii inatupilia mbali shauri lililofunguliwa", alisema Jaji Polk katika uamuzi wake.

CHAMBERS hawezi kufugua kesi upya balianaweza kukata rufaa. Anasema bado anatafakari kwa makini uamuzi huo ili kujua kama atakata rufaa au la.

Alifungua kesi hiyo mwaka jana (2008), na kwamba alisema, "Mungu alikuwa amesababisha vifo vingi na uharibiifu na ugaidikwa mamilioni ya wakazi wa dunia."

CHAMBERS alisema, "Mahakama ilijua kuwepo kwa MUNGU na yote ayafanyayo kiasi cha kujua uwezo wake wa kujua yote. ALHAMDULLILLAH. Kwa vile MUNGU anajua kila kitu, basi ni wazi kuwa atakuwa anajua kwamba kuna shitaka hili dhidi yake." (inna lillahi wa-inna illaihi raj-uun).

Seneta huyo wa NEBRASKA kwa miaka 38, alinukuliwa akisEma alifungua shitaka hilo ili kutoa ujumbe kuwa mtu yeyote anaweza kumshitaki yeyote akiwamo MUNGU. ASTAGHFIRRULLAH!.

1 comment:

  1. SIO VIZURI KUDILI NA MAMBO TUSIYOYAJUA KUHUSU MUNGU TUSIJE TUKAKUFURU BURE.

    ReplyDelete