Friday, May 8, 2009

SWALA YA IJUMAA MSIKITI MKUU WA WASHINGTON DC

Wandugu leo hii niwaletee ya Msikiti mkuu wa Washington uitwao "Washington National Mosque." Ndio nimetoka huku muda huu huu kuswali swala ya Jamaa ya leo hii Mei 8, 2009. Alhamdullillah.

Swala yetu leo Khutba yake ilitilia mkazo Upwekeshaji wa Mola wetu, kumjua Mjumbe wake na kujali familia; hususan wazazi wetu. Kwamba endapo hutatenda wema kwa wazazi, basi huwezi kujisifu kuwa unamjua Mtumbe wetu (S.A.W.) na vivyo hivyo endapo hutomjua Mtume wetu ni dhahiri kwamba na Mola wetu hutakuwa karibu naye. Hivyo tumeaswa sana katika mambo haya.

Baada ya Swala (kiasi cha saa nane na nusu mchana) kama kawaida katika msikiti huu, kulikuwa na chakula cha mchana. Leo kulikuwa na wali wa mboga na mchuzi wa nyama ya mbuzi, pamoja na mikate. Tukahudhuria katika sadaka hiyo, alhamdullillah. Japo hatukuwa watu wengi kiasi kwamba sehemu ya chakula ilibakia. Nikawakumbuka ndugu zangu nyumbani Tanzania na kujiuliza wakati huu sijui huko wanakula nini? Najua ni kipindi cha masika na hivi karibu mahindi ya kuchoma yatakuwa mengi tu.

No comments:

Post a Comment