Friday, November 30, 2012

MHADHIIRI IMAN PETRO AFARIKI DUNIA DAR ES SALAAM, TANZANIA

Kwa mujibu wa taarifa niliyoipokea kutoka kwa mjumbe wa BARAZA KUU la Jumuiya na Taasisi za Kiislam,
Br. Ally Mbaruku
Ndugu yetu katika Iman,

IMAN  PETRO  AMEFARIKI  LEO JUMATATU NOV 26, 2012, BAADA YA SWALA YA MAGHARIBI,

Taratibu za maziko sikuzipata, anaejuwa atujulishe tafadhali
 
Marehemu katika uhai wake alikuwa na juhudi kubwa ya Dini
Aliwahi kurudishwa Bara kutoka Zanzibar kwa nguvu za Dola
Iman Petro ni mtu aliesilimu akitokea katika Ukristo, na aliugua ugonjwa usiojulikana kwa muda kiasi,

Baadhi ya Wahadhiri wanahisi kaumizwa na sumu kutoka kwa maadui wa Dini ya ALLAH, Maana Lecture  zake zilikuwa TISHIO
Tumuombe Mwenyezi Mungu amghufirie dhambi zake ndugu yetu na amtie katika pepo yake
 
 
INNAA LILLAAHI WA INNAA ILAYHI RAAJIWUUN
Wasalam
Pazi Mwinyimvua

1 comment: