Ugombolwa wafunga machinjio
ya nguruwe
na Betty Kangonga
Tz Daima 18 Nov 2012
UONGOZI wa Serikali ya Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya
Segerea, Wilaya ya Ilala, imeyafunga machinjio ya nguruwe kutokana na
wamiliki hao kukiuka taratibu za kisheria.
Akizungumza jana mara baada ya kufanya ziara ya
kushitukiza katika machinjio hayo yaliyopo katika eneo la makazi, Ofisa
Mtendaji wa mtaa huo, Mathew Mayonga aliyeambatana na uongozi wa mtaa huo,
alisema amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha na ukiukwaji wa taratibu.
Alisema kuwa amelazimika kuyafunga machinjio hayo na
kuwasilisha zuio la mahakama kutokana na uongozi wa mtaa huo kutokuwa na
taarifa juu ya uwepo wa machinjia hayo katika eneo hilo.
“Yaani naomba kuanzia sasa msimamishe zoezi la
uchinjaji na muuze nyama zilizokwisha andaliwa…na kama mtakiuka utaratibu huo
nina hakika nitapata maelezo na hapo ninajua nini hatua ya kuchukua,”
alisema.
Mayonga, alisema kuwa wamiliki hao hawana nyaraka
zozote zinazowahitaji kufanya shughuli hiyo hivyo hata uandaaji wa nyama hiyo
unaweza kuwa na dosari.
Alisema baada ya kukagua mazingira yanayolizunguka
eneo hilo alibaini utitirishwaji hovyo wa maji machafu ambao umekuwa kero kubwa kwa
majirani wanaoishi eneo hilo.
“Mnawezaje kufanya kazi wakati hakuna nyaraka
zinazowataka kufanya hivyo kwa kweli naomba msimamishe haraka hadi
mtakapopata barua rasmi la kutakiwa kufanya shughuli hiyo,” alisisitiza.
Naye
Mwenyekiti wa mtaa huo, Mariam Machicha, alisema kuwa hiyo ni mara ya pili
kufika katika eneo hilo na mara ya kwanza walilazimika kulifungia eneo hilo
lakini wakashangaa kwa kufunguliwa tena.
“Hii ni mara ya pili nafika hapa…mara ya kwanza
tulilifunga lakini cha ajabu likafunguliwa kinyemela,” alisema
Akijitetea Katibu wa Umoja wa wadau wa nguruwe Manispaa ya Ilala, Daudi Charles, alisema kuwa ofisa mifugo wa wilaya hiyo aliwataka kuendelea na biashara hiyo huku akiendelea kuwatafutia vibali.
Akijitetea Katibu wa Umoja wa wadau wa nguruwe Manispaa ya Ilala, Daudi Charles, alisema kuwa ofisa mifugo wa wilaya hiyo aliwataka kuendelea na biashara hiyo huku akiendelea kuwatafutia vibali.
No comments:
Post a Comment