Assalaam alaykum.
Allah anatuambia katika Qur'an "Na
hawatoacha kukupigeni vita mpaka wakuritadisheni kutoka kwenye dini yenu
wakiweza.." (Al Baqarah 2:217)
Siku ya Jumamosi terehe 24 Novemba,
2012 itaingia katika maisha yangu ya da’wah kama siku niliyoona kivitendo jinsi
ambavyo mipango iliyowekwa na wakristo kupitia mafunzo maalum yaitwayo “Evangelizing
Muslims” inavyoweza kuwatoa waislamu kutoka katika Uislamu wao.
Nilialikwa kuhudhuria sherehe za
ufungaji wa shule ya Kiislamu Iqra English Medium School inayoendeshwa na Pahi
Islamic Center, taasisi iliyosajiliwa yenye Makao yake Makuu kijiji cha Pahi, Tarafa
ya Pahi, Wilaya ya Kondoa yenye waislamu takriban 95%. Kondoa kuna vijiji
huwezi kukuta mkristo hat ammoja lakini hivi sasa kuna kasi kubwa ya
kuwaritadisha waislamu.
Ninaambiwa kwamba mnamo miaka ya
1998-2000, walifika wazungu watatu wakiwemo Wamarekani wawili (wanawake) na
Mjerumani mmoja. Walifika wakidai kutaka kujifunza lugha na mila za kabila la warangi.
Wakapokelewa na ndugu mmoja aitwaye Halifa Nchasi (ambaye sasa ndiye Katibu wa
Pahi Islamic Center) na ndugu huyu akawafundisha hawa wazungu kirangi kwa muda
wa wiki tatu na wakakimudu vizuri (walikuwa wataalam wa lugha).
Wale wanawake walifikia kuishi
maisha ya mwanamke wa kawaida wa kirangi wakishiriki shughuli zote zifanywazo
na mwanamke wa kabila hili kuanzia kuteka maji, kukata kuni hadi kubeba mtoto
mgongoni na wakapewa majina ya kirangi-mmoja akiitwa Mwasu na mwingine Sware. Baada
ya muda, jamaa hawa wakaja kuanzisha mradi uitwao “COMPASSION” ambao ulilenga
kuwasaidi awaislamau masikini husuusan katika huduma ya afya.
Wakaanza kumimina misaada kutoka
huko ughaibuni wakianzia na kuweka magari matatu katika vijiji vitatu- moja
pahi kwenyewe, jingine Kinyasi na jingine Salare kwa ajili ya kubeba wagonjwa
kwa kila mwenye mgonjwa kuchangia fedha ya mafuta tu Sh 10,000 kuepelekewa
mgonjwa wake hospitalai ya Wilaya Kondoa mjini kwani tarafa nzima ya pahi haina
hospitali. Wapashajai ahabari wangu wananiambia kwamba mara baada ya waazungu
hawa kuja Pahi, malaria ya ajabu ilizuka. Wanaamini kwamba wazungu hawa
walipandikiza mbu mwenye vimelea vya malaria.
Baadaye wazungu hawa wakaomba
kupataiwa ekari 7 ili wajenge zahanati hapo Pahi. Uongozi wa serikali ya kijiji
ukaitish amkutano wa hadhara na kuwataka ushauri wanakijiji ambao 99% ni
waislamu. Kutokana na “wema” waliofanyiwa, wanakijiji wote wakaunga mkono
wakristo hao kupatiwa ardhi waliyoomba. Wakrsito wakajenga zahanai yao na ikawa
pia andiyo kituo cha kuwakusanya wale waislamu masikini kwa ajili ya mafunzo
maalum kila jumamosi ambapo wakitoka huko hupatiwa mche wa sabuni, madaftari
n.k.
Kilichofuatia ni jamaa kuomba
atrdhi nyingine ekari 7 kwa ajili ya kujenga shule ya wasichana. Hivi sasa
wanaendesha shule ya wasichana (boarding na day) yenye kuchukua wasichana 600
na kila mwaka ninaambiwa takriban wasichana waislamu 5-10 huritadi. Hata wale
amabo hawajaritadi, huonesha wazi kuwa wameugura Uislamu kwa sababu wanapopita
njiani wakawaona waislamu husuusan akina mama waliojisitiri husikika wakisema “Mashetani
hao”.
Kubwa zaidi hiyo COMPASSION
imeanzisha mtindo wa “Family Friends” ambapo familia moja masikini ya kiislamu
huunganishwa na familia ya kikristo huko Ulaya ana Marekani na hiyo familia ya
nje huisaidia familia ya ndani kwa hali na mali. Hili nalo limezidisha hatarii
ya waislamu kuritadishwa na tayari familia kadhaa zimesharitadi familia nzima.
Kibaya zaidi, waislamu hapo Pahi
wamegawanyika wakipigana vita. Answar Sunnah wamegawika makaundi mawili yenye
kupingana na hawa wanaosema wao ni Bakwata pia ni faraqa tu. Hali ya Paahi na
vijiji vingi vya Kondoa ni mbaya. Kingine cha kuzingatia Kondoa sasa ni Jimbo la
Kanisa Katoliki lenye Askofu wake kamili.
Nimefanya fikra na waislamau pale
na ndugu zetu wa Morogoro kwa ajili ya kuunusuru Uislamau pale. Yapo yaliyoazimiwa
ambayo siwezi kuyaweka bayana humu bali niwatangazie tu biashara kwamba wale
wenye Ilmu wanaaweza kuitembelea Pahi na kufanya da’wah. Pia wale ambao hatuna
Ilmu, ikifikia wakati nguvu zikahitajika nasi tuwe tayari. Pahi imetengewa Tshs
10,000,000 kila mwaka kwa ajili ya kuritadisha waislamu.
Inasemekana wazungu hawa walisoma
kwenye Mtandao kwamba Paahi ni Markaz Kuu ya Fisabiylillahi Marakaz barani
Afrika. Ni kweli pahi kulifunguliwa Markazi Kuu ya Fiysabiilillahai Afrika mwaka
1981. Hadi sasa kuna ekari 110 zimekaa tu pasina kutumika mbali na msikiti
uliowekwa jiwe la msingi na aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo Mzee Aboud
Jumbe. Huu naoa ni udhaifu mkubwa wa taasisi hiyo. Pia kuna taasisi nyingine
iitwayo IDA inazo ekari 16 nazo zimelala pasina kufanayika chochote hapo kwa
miaka sasa. Watu wako tayari kinachokosekana ni uongozi na maelekezo.
Huu ni mfano tu kwani najua hali
ndiyo hii sehemu kubwa ya nchi. Ukizingatia kwamba wakristo wana hiyo MoU yao
na Serikali kutengewa mabilioni kwa ajili ya elimu, afya na huduma nyingine za
jamii, bila shaka kasi ya kuwaritadisha waislamu itaongezeka.
--
Sheikh Muhammad Issa
(Private Mail)
Youtube Channel" Mohamed Issa
I had very small penis, not nice enough to satisfy a woman had many relationship called off it became an embarrassment which i couldn't afford to bear no more because i had so e relationship called off because of my situation, then I started searching for solutions cause I knew if I didn't find a solution it would eventually end my sex life then I came across saw some few comments about Dr Ekpen then decided to email him on so I decided to give his herbal product a try then we discussed, he then gave me some comforting words and also gave his herbal cream for Penis enlargement cream and pills, Within 7 days of usage of it, i began to feel the enlargement of my penis, and now after 2 weeks of using his products my penis is about 10inches I couldn't wish for anything in life other than to be free from this predicament and Dr Ekpen medication gave me the Result I badly needed longer email him to get your issue solved just like he solved mine contact (Email: doctorekpen222@gmail.com) or whatsapp +2348102454875 also have cure to all kind of diseases
ReplyDelete