Imebandikwa hapa leo hii 17/11/2012.
Assalaam alaykum.
Umekurubia
kuingia mwezi wa Muharram, miongoni mwa miezi mitakatifu katika Uislamu
iliyofuatana ambayo ni miwili kabla ya huo ujao (Dhul Qaadah na Dhul
Hajji) na kisha mwezi wa Rajab. Katika mwezi huu wa Muharram, Mashia au
Rawaafidhwah hufanya sherehe zao za masiku kumi ya Muharram ziitwazo
Sherehe Ashuura.
Mashia wanaitwa pia Rawaafidhwah kwani jina
hili kalitaja mmoja wa ma-Sheikh wao Almajlisy katika kitabu chake
(Bihaarul-anwar) akasema katika mlango aliouita, mlango kuhusu (
Ubora wa raafidhwa na uzuri wa kujiita jina hili), kisha akataja kutoka
kwa Sulaiman Al-aamash kuwa amesema: niliingia kwa Abii Abdillah
Jaafar bin Muhammad nikasema kumwambia: Hakika watu wanatuita
Raafidhwa, nini maana ya Raafidhwa? Akasema: wallwahi sio wao
waliokuiteni hivyo bali Mwenyezi Mungu alikuiteni hivyo katika Taurati
na
Injili kupitia ulimi wa nabii Mussa na nabii Issa.( Tazama kitabu (Bihaarul-anwar) cha Almajlisy 65/97. (ambacho ni miongoni mwa marejeo yao muhimu katika vitabu vyao
vya sasa)
Na imesemekana kuwa: wameitwa raafidhwa kwa sababu
walikuja kwa Ally bin Hassan wakamwambia: Jitenge na Abubakari na Omar
ili tuwe pamoja nawe, akasema: wao ni vipenzi wa Babu yangu, siwezi
kujitenga nao bali niko pamoja nao, wakasema: hivyo basi tumekukataa,
ndipo wakaitwa Raafidhwa, na akaitwa kila aliyemuunga mkono Zaid kuwa ni
Zaydiyya.(Rejea: Attaaliqaat alaa matni lum-atul iitqaad cha Sheikh Abdallah Aljibriin uk.108).
Na
inasemekana:wameitwa Raafidhwa kwa kupinga kwao utawala wa Abubakari na
Omar (Radhi za Allwah ziwe juu yao) -Tazama Maqaalaatul-Islaamiyiin cha
muhyiddiin Abdulhamiid (1/89) na imesemekana: Wameitwa hivyo kwa kukataa kwao Dini. (Tazama Ibid 1/89)
Kwa
hiyo Mashia au Rawaafidhwah ni pote jengine kabisa mbali na Ahlu Sunnah
wal Jamaa lakini waislamu wengi wanaojinasibu na Ahlu Sunnah wal Jamaa
wamekumbwa na itikadi za Kishia na miongoni mwa hizo ni sherehe zao za
Ashuura katika mwezi huu wa Muharram ambapo hukumbuka kifo cha Al
Hussein Ibn Ali (Radhi za Allwah ziwe juu yake na Baba yake pia). Shubha
inayopataikana hapa ni kwamba siku ya Ashuura imethibiti kwa hadithi za
Mtume (Rehma na Amani ziwe Juu lake) alopofika Madinnah ana kuwakuta
Mayahudi wakiadhimisha siku hii ambayo ni terehe 10 Muharram. Akawauliza
ni siku gani hii mnayoiadhimisha? Wakasema ni siku Allwah alipomuokoa
Musa na watu wake dhidi ya Firauni. Mtume akawaambia sisi ndio bora kwa
Musa kuliko nyie. Hapo Mtume (rehema na amani ziwe juu yake) akamuarisha
swahaba awatangazie watu kuwa yeye atafunga swaumu siku hiyo na iliyo
kabla yake yaani "Yawmu Taasu'a".
“Ashura”: Hii ni ile siku ya mwezi kumi Muharram (Mfunguo nne) na “Taasuaa”:
Hii ni siku ya mwezi tisa Muharram. Dalili na ushahidi wa usuna wa kuzifunga
siku mbili hizi ni ile hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Abbas-Allah awawiye
radhi-“Kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alifunga siku ya
Ashura na akaamrisha watu kufunga”. Bukhaariy [1900] & Muslim
[1130]-Allah awarehemu.
Kwa
hiyo kilicho Sunnah ni kufunga siku ya tarehe 9 na 10 Muharram kama
alivyofanya Mtume (Rehma na amnai za Allwah ziwe juu yake) kinyume na
wafanyavyo Mashia/Rawaafidhwah wafanyavyo kwa kuzifanya siku hizi za
vilio na kujipiga miili hadi kutoka damu eti kwa kukumbuka kuuwawa kwa
al Hussein Ibn Ali (Radhi za Allwah ziwe juu yake na baba yake Ali Ibn
Abi Twaalib).
Itikadi
za Mashia kuhusu kuuwawa al Hussein ibn Ali (ambazo ndiyo chimbuko la
Sherehe zao za Ashuura/Muharram) zimewafikisha hata kukufuru juu ya
Allwah na matukufu yake. Kwa mfano, Mashia
wanaitakidi sehemu yalipo makaburi ya watu waliodai kuwa ni maimamu
wao, au ambao ni maimamu kweli, kwa sehemu hizo ni sehemu takatifu,hivyo
Alkuufa ni haram(sehemu takatifu),pia Karbalaa ni haram,na Qumm nayo ni
haram. Na wanayo riwaya wanayo dai kuwa imepokelewa kwa Asswaadiq
kwamba, Mwenyezi mungu anayo haram yake ambayo ni makka,na Mtume wake
anayo haram yake ambayo ni Madina,na amiiril-mu`uminiina anayo haram
yake ambayo ni Alkuufa,na sisi tunayo haram yetu ambayo ni qumm.
Na Kar-balaa kwa Mashia ni bora kulikko Alqaaba. Imekuja katika kitabu(Bihaarul-anwar)kutoka kwa Abii Abdillah kwamba kasema;
"Hakika
Mwenyezi mungu aliiteremshia Alqaaba wahyi (ufunuo) lau kama si udongo
wa Kar-balaa nisingelikufanya bora ,na lau kama si mwili wa
yule aliyeko katika udongo
wa Kar-balaa nisingekuumba,wala nisingeumba nyumba ambayo kwayo
umejifakharisha,basi tulia na uwe ni Mkia
dhalili na si mwenye kibri kwa ardhi ya kar-balaa,la sivyo nitakutupa katika Jahannam" (Rejea kitabu Albihaar 10/107).
Bali
Mashia/Rawafidhwah wanaona kuzuru kaburi la Husein huko karbalaa ni
bora kuliko nguzo ya tano ya uislamu(Hijja)!!. Amesema Almajlisykatika
kitabu chake (Bihaarul-anwar)Kutoka kwa bashiir addahaan
amesema;"Nilimuuliza Abuu Abdillah(a.s) Endapo itanipita hijja
alafunikaenda katika kaburi ya Husein? Akasema:Vizuri sana ewe
Bashir,muumini yeyote atakae liendea kaburi la Husein hali ya
kutambuahaki yake,katika siku ambayo sio siku ya idd,basi huandikiwa
thawabu za Hijja 20 na Umra20 zenye kukubaliwa,na thawabu za kushiriki
katika vita 20 vya Jihadi pamoja na Mtume au Imamu muadilifu, na atakaye
liendea siku ya Arafa hali ya kujua haki zake basi huandikiwa thawabu
zaHijja 1000 na Umra 1000 zenye kukubaliwa,na thawabu za kupigana Jihadi
1000 pamoja na Mtume au Imamu muadilifu.
Hivyo
ndugu katika Imaan, mnawezakuona ni jinsi gani Mashia/Rawaafidhwah
wanavyomtukuza la Hussein mjukuu wa Mtume (rehma na Amani ziwe juu yake)
na Karbalaa ambapo ndipo alipouawa kwa dhulma kiasi cha kufifisha
Arafa, Hijja kwa ujumla na Al Kaaba yenyewe. Si ajabu tena kuwaona
vijana wao wakijipiga kwa minyororo na kuvuja damu wakiamini kuwa
wanapaswa kujiadhibu hapa hapap duniani kwa kushindwa kumnusuru Al
Hussein siku ile aliyouawa.
Haya
tunayaleta huku tukijua kuwa kuna miito ya Umoja na Mshikamano wa
Waislamu pasina hata kujali tofauti za kiaqeedah baina yetu. Miito hii
ingawa ina lengo zuri lakini kupitia kushikamana huku hata na watu wa
baatwili, aqeedah sahihi ya Ahlu Sunnah wal Jamaa inatoweka na sote
tunajikuta tukiuvaa Ushia pasina kujua. Baada ya haya tunataraji
wale wenye chembe chembe za Ushia watakuja juu labda waogope
kujidhihirisha. Kwa wengi haya yanawezakuwa hayana uzito wowote kwani
kwa zama za leo ambapo ujaahili wa kutokujua dini umedhihiri na kuweka
mbele mas'lahi ya dunia, suala la aqeedah sahihi si jambo muhimu kwao.
Tumeleta haya ili iwe kama alivyosema Allwah (Subhaanahuu wa taala);- "Ili
aangamie mwenye kuangamia kutokamana na bayana na ahuike mwenye kuhuika
kutokamana na bayana" (8"42). Aaangamie kiimani naahuike kiimani.
TUJIEPUSHE NA ITIKADI ZA KISHIA KATIKA MWEZI WA MUHARRAM TUSIJE KUANGAMIA.
Allwah ndiye Mjuuzi zaidi,
Ndugu yenu katika imaani,
Muhammad Issa
No comments:
Post a Comment