Thursday, August 9, 2012

MSIMAMO WA WAISLAM WA TANZANIA JUU YA SENSA 2012 No. 2

Thursday, 9 August 2012, 1:17 Subject: [tz_muslim_community] TAARIFA MUHIMU KWA UMMAH Assalaam alaykum warahmatullahi. Kuhusu msimamo wa waislamu kutokushiriki sensa, Hay-atul Ulamaa ilikaa na makamishna wa Tume ya Sensa wakiongozwa na Hajjat Amina Said na pia Mkurugenzi Mkuu wa Sensa tarehe 30 Julai, 2012 kuzungumzia msimamo wa waislamu wa kutokushiriki sensa ya mwaka huu hadi kipengele cha dini kiwekwe kwenye dodoso la sensa. Kikao chetu kiliwafumbua mengi wajumbe hao na wakaona uzito wa hoja za waislamu. Waliahidi kuwa wanayapeleka juu kwa maamuzi kwa sababu wao si wenye maamuzi na kwamba watakuwa (wao watu wa serikali) na vikao vya juu kuanzia tarehe 4 Agosti, 2012. Sasa tumekuwa tukipata maswali watu wakituuliza "Sheikh mmefikia makubaliano gani katika kikao chenu cha pili na watu wa sensa?". Tunapenda kuwaarifu waislamu mambo yafuatayo;- Mosi, Hay-atul Ulamaa imekaa kikao kimoja tu na watu wa sensa na hakukuwa na kikao cha pili. Pili, Madai yetu hayakuwa tu kuweko kwa kipengele cha dini, bali pia uangalizi wa waangalizi waislamu na wakristo kwa sababu takwimu zinazotolewa zina utata na kila upande unadai wao ni wengi. Hili lilikuwa kujaribu kuzuia kuchakachuliwa kwa matokeo ya kipengele hicho. Pia dai letu jingine ni kwa kuwa muda umekwenda, basi sensa isogezwe mbele kuruhusu waislamu kujiandaa baada ya kuwahamasisha wasishiriki. Tatu Hadi sasa serikali haijatoa msimamo kuhusu kuweko kwa kipengele cha dini katika dodoso la sensa kama madai yetu yalivyo. Tunachoshuhudia ni Rais kuendelea kutoa msimamo wa serikali kama hivi majuzi alipokuwa Loliondo alisema "Hatuhesabu watu kwa mujibu wa makabila yao wala dini zao" (ITV, TBC1). Nasiki ana PM nae, leo asubuhi katika maswali ya papo kwa hapo ameulizwa swali na amesema "serikali haitoweka kipengele cha dini". Nne: Waislamu hatukuw ana matumaini ya kusikilizwa na serikali kwa sababu ni kawaida kwamba waioslamu hawasikilizwi mpaka mitulinga itumike kama vile maandamano n.k. Na msimamo wa kutokushiriki sensa ni katika utamaduni huo huo. Tano: Kuna ombi la Ikulu kukutana na Rais mwanzo wa wiki ijayo kuzungumzia hili. Ukiangali atrend hii, utaona juhudi zote za serikali ni kama "Delaying tactic" kufanya waislamu wa-relax kwa kutaraji kutakuw ana mabadiliko. Kwa kweli mimi ni mtu wa mwisho kuamini kwamba waislamu tutasikilizwa. Hay-atul Ulamaa itakwenda kumsikiliza Rais atasema nini. THE BALL IS IN THEIR COURT. Msimamo wa masheikh ni ule ule, WAISLAMU HATUHESABIWI HADI MASHARTI YAUSHIRIKI WETU YATAKAPOTIMIZWA. Naomba myajue yote haya na muwafikishie na watu wa makundi yetu mengine ili na wao wawe na taarifa hii. Allwaahu Al-musta'aanu. Maassalaam.

No comments:

Post a Comment