Isihaka Mchinjita posted in INTER ISLAMIC SCHOOLS TZ -20/8/2012
Mkuu wa wilaya kilwa, Mkoa wa Lindi, anusurika kupigwa Kilwa Kivinje
Mkuu wa wilaya ya Kilwa ametolewa msikiti wa Al az har, mjini Kivinje chini ya ulinzi wa
viongozi wa msikiti baada ya kuwataka waislamu kushiriki sensa.
Awali mkuu huyo wa wilaya alichangia Tsh.1,000,000 kwa ukarabati wa msikiti ambapo baadae alibeza
msambazaji wa vipeperushi vinavyowataka waislamu kutoshiriki sensa mpaka
kipengele cha dini kiwekwe.
Baada ya kauli yake hiyo waislamu walinyoosha mikono msikiti mzima wakitaka kumhoji.kufuatia hali hiyo viongozi walisimama kutaka kuzuwia hali hiyo na hapo zogo likatokea na mashekh kuamua kumtoa mkuu huyo huku wakilaumiwa na waumini na hivyo kuondoka msikitini hapo bila hata kuomba duwa.
Hali hii imemfanya mkuu wa wilaya kutozungumzia sensa baadae alipokuwa kwenye Baraza la Eid el Fitr, ambapo pia alialikwa kama mgeni rasmi.
HIZI NI SALAM TOSHA KWAMBA WAISLAM WA KILA KIVINJE WAMESIMAMA KIDETE KUTETEA DINI YAO NA KUONDOA MUNKAR KWA MIKONO YAO.
Tuesday, August 21, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment