Sunday, August 19, 2012

KUMPINGA KADHI SI KUTOKA KATIKA UISLAM TANZANIA

 SHEIKH  JUMA  MBUKUZI JUU YA  KUMPINGA  KADHI -  19/8/2012

Re. Kumpinga Kadhi ni kujiengua Uislamu - Muft Simba

Assalaam aleikum ndugu yangu Pazi.
Mufti kwa fatwa aliyoitoa kajiingiza ukafirini mwenyewe, kwa sababu mtu anapomwita mwingine kafiri na huo ukafiri usipothibiti kwa huyo mtuhumiwa, basi kwa kauli ya Mtume s.a.w ukafiri unamrudia na kumthibitikia huyo mtuhumu mwenyewe. Hapa waisilamu hatujapinga kadhi kuwepo, kwa sababu ni sisi ndio tuliopiga makelele kumdai huyo wala sio yeye mufti na bakwata lake. Kinachogomba ni uhuni uliotumika kumsimika kadhi wa bakwata badala wa kadhi wa waisilamu na kumkataa kadhi wa bakwata hakumkufurishi mtu. Mufti kimakamo ni mdogo sana kwa kadhi, iweje huyu mdogo amteuwe mkubwa sio sahihi. Mufti kavunja makubaliano ya shura ya pamoja ya waisilamu akafuata uamuzi wa kibabe yeye na bakwata yake, hiyo ni khiyana inayomuingiza katika unafiki. Hivyo asitutishe na ukafiri usiokuwepo kwetu lakini uko dhahiri kwao. Kuhusu sensa, kikundi kidogo kimefanya kazi nzuri sana mpaka mafisadi wa amani yanchi wakiongozwa na mkurugenzi wa TBC wamekiri uovu wao hadharani na kuomba msamaha, huu ni ushindi mkubwa, uliotokana na juhudi ya wachache na taufiq ya Allah, kwani vikundi vingapi vidogo vimeshinda makundi makubwa kwa idhini ya Allah. Hivi kweli watu hata wakiwa wachache basi waonelewe na wasipewe haki zao ?, mbona majirani zetu, ambako kuna waisilamu wachache zaidi kuliko hapa Tanzania, huko waisilamu wanasikilizwa, kuheshimiwa na kupewa haki zao. Tatizo hapa kwetu inaonyesha ni ubarakala wa bakwata na mufti wao, wakishashiba wao futari kusahau haki za wengine. Kwa nini yeye mufti atoe fatwa nzito kama hiyo kwenye futari ya Halifa Hamisi ?, kwa nini asiliite jopo la ulamaa aliloliunda na kuwapa vitisho hivyo, yeye na Halifa Hamisi wake wote sio wakweli.

No comments:

Post a Comment