Friday, April 3, 2015

MASJID HARAM MOSQUE IN MAKKATUL MUKKARAMA, SAUDI ARABIA [KIPEPERUSHI]

KIPEPERUSHI CHA  MAKTABA YA  MASJID  HARAM  [MSIKITI MKUU] ULIOKO  MAKKA, SAUDI  ARABIA  [LIBRARY OF MASJID  HARAM,  MAKKA]

www.gph.gov.sa
www.quranholymosque.com

KIPEPERUSHI HIKI KINAPATIKANA KATIKA MAKTABA YA MASJID  HARAM WA MAKKA KATIKA LUGHA YA KIARABU.   

 NAKINAKILI HAPA KIKIWA KIMETAFSIRIWA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI.  

MFASIRI:   Sheikh  Mohamed  Nassor  Zahor Al-Kindy  wa  Al Hail,  Muscat,  Oman.

Kwa faida ya  Wasomaji wanawake,  Maktaba hii ya  Msikiti Mkuu wa Makka [Masjid Haram] hufunguliwa kwao siku za
 ALHAMISI :   Kuanzia saa  10.00 jioni hadi saa 1.00 usiku
JUMAMOSI:   Kuanzia saa   10.00 jioni hadi saa 1.00 usiku

Kwa mahujaji wanawake  wa kutoka Afrika ya Mashariki au wanaofahamu lugha ya Kiswahili, taarifa hii itawasaidia kufahamu muda huu mahsusi uliotengwa na Maktaba hii kwa ajili ya wasomaji wanawake.

Maktaba hii inafikiwa kwa kuingia KING FAHD  GATE No.  79,  KING FAHD STAIR  80, katika Masjid Haram.

Yafuatayo ndio  yaliyoandikwa katika KIPEPERUSHI hicho nilichokabidhiwa mkononi na Wakutubi wa Makataba ya Masjid Haram mwezi wa 10, 2014; kupitia kwa Kiongozi wangu aliyenisindikiza huko  Maktaba, Bw. Haji Makame Haji  wa simu Na. 0787 554491, Zanzibar.
.

JINA:   RUQIYA  SHAR'IA


Ukurasa wa Kwanza:   Sura Al-Faatiha kamilifu.
                                      Sura Al Baqara: 1 - 5, 102, 109, na 137.

Ukurasa wa Pili:  Sura  Al  Baqara:  Aya  ya 164, 255, 285, 286.
                              Sura Al Imraan:  Aya  ya 190, 191.
                              Sura Al Nissaa :  Aya  ya 54. 

Ukurasa wa  Tatu:  Sura  A'Raaf:   Aya ya  54, 55.
                                 Sura Al Tauba:  Aya ya 14, 26, 40
                                Sura  Al A'Raaf:  Aya ya 117, 118, 119.
                                Sura   Younis:   Aya ya  79, 80, 81
                                Sura   Is'raa:  Aya ya 82.
                                Sura  Twaha:   Aya ya  65, 66, 67, 68. 69.

Ukurasa wa Nne:   Sura   Al Mu'minun:  Aya ya 115, 116, 117, 118
                                 Sura  Shyaraa:         Aya ya 80. 
                                 Sura  Aswafat:          Aya  ya 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10.
                                 Sura  Fussilat:          Aya  ya 44.
                                 Sura   Al Ahqaaf:        Aya ya 31.
                                 Sura  Al Fat'h:           Aya  ya 26.
                                 Sura  Al Rahmaan:   Aya ya 31, 32, 33. 34.

 Ukurasa wa Tano: Sura   Al Hashr:          Aya ya 21, 22, 23.
                                 Sura  Al Qalam:        Aya ya 51.
                                 Sura  Al Kafirun:       Aya ya 1, 2, 3, 4, 5, 6.
                                 Sura  Al Ikhlaas:        Aya ya 1, 2, 3, 4. [Qul-huwa Allahu Ahad]
                                 Sura  Al  Falaq:          Aya ya 1, 2, 3, 4, 5. [Qul-Audhubirabil Falaq]
                                 Sura  Al Naas:            Aya ya 1, 2, 3, 4, 5, 6. [Qul-Audhubirabinaas]

Ukurasa wa Sita:     DUA  ZITUMIKAZO:

A -  AUDHU BILLAHI  ASAMIU AL ALIM MINA SHAITWANI AL RAJIM 
       MIN HAAMAZIH  WA NAFAKHIHI WA NAFATHIHI

B - AUDHU BI KALIMATI LLAH WA ALTAAMATI MINI SHARI MA KHALAQA.

C - AUDHU BI KALIMATI LLAH ALTAAMATI MIN KULI SHAITWANI WA HAAMMAH WA MIN KULI AINI L'LAMMAH.

D - AUDHU BI KALIMATI  LLAHI ALTAAMATI ALATI LAA YUJAWIZUHUNNA BARAN WA  LAA FAJIR  MIN  SHAARI MAA YANZILU MINA SAMAA WA MIN SHARRI  MAA
YA'RUJU  FIHA WA MIN SHAARI MAA DHARA'A  FIL AL ARDH WA MIN SHARRI MAA YAKH'RUJU MIN HAA WA MINA FITAN AL- LAYLI WA AL NAHAAR WA MIN SHARRI
TWA'WARIQU AL-LAYLI WA ALNAHAAR ILA TWARIQAN YAT'RUQU BIKHAIR YAA RAHMAAN.  

E - AUDHU BI KALIMATI LLAH AL TAAMATI MIN GHADHABIHI WA IQABIHI WA MIN SHARRI IBADIHI WA MIN SHARRI  HAMAZATI SHWAYATIN WA ANN YAHDHURUN.

F -  BIISMILLAHI AL RAHMAANI ALRAHIM

G - BISMILLAHI ARQIKA MIN KUULI SHAY'I YUU'DHIIKA WA MIN SHARRI KULU NAFSI AU 'AINI HAASID  ALLAH YASH'FIKE BISMILLAH ARQIKA

H - BISMILLAH AL'LADHI LAA YADHURU MA'A ISMIHISHAY FI AL'ARDHI WALA FI  AL'SAMAA WA HUWA ALSAMIU AL ALIMU  (x 3)
I - HASBI ALLAHU LAA ILAHA ILLA HUWA ALEIHI TAWAKALTU WA HUWA RABI AL'ARSHII AL ADHIM (x 7).   


Ukurasa wa Saba: 


J - AS'ALU LLAH AL  ADHIM RABI AL AR'SHI AL ADHIM AN YUSH'FIKE (x 7)

K - ALLAHUMAH RABI NNASS ADH'HEB ALAS WA ASH'FI ANTA ALSHAFI LAA SHIFAA ILLA SHIFAUKA SHIFAA LAA YGHADIRU SAQAMA.

L - ALLAHUMMA INNI AUDHU BI WAJHIKE AL KARIM WA KALIMATIKE AL TAAMATI MIN SHARRI MAA ANTA AKHIDHU BINASSSIYATUKA ALLA HUMAH ANTA TAKSHIFU AL MAGHRAM WA ALMAATHAM ALLAHUMMAH INNAHU LAA YAHZAMU JUNDUKE WALAA YUKHLAFU  WAADUKA  SUBHANAKA   WA BIHAMDIKA 

M* - [YADHAU YADAHU  ALAA MAUDHI AL ALAM WA YAQUL]:-  BISMILLAH x 3 AUDHUBILLAHI WA KUDRATIHI MIN SHARI MA AJIDUWA UHADHIRU x 7.


Ukurasa wa  Nane:

  ILAJI (MATIBABU) YA SIHIRI, KIJICHO NA HASAD:- 

1.   Kutenda yaliyokuwa  wajibu na kuepuka yaliyo  haramishwa  na kutubu makosa yote. 
2.  Kutubu toba ya kweli na kurudisha haki za watu 
3.  Kusoma Qur'ani kwa wingi kila siku 

4.  Kujikinga  kwa kusoma Dua na Muawadhati [Qul-huwa llahu ahad; qul auhu birabi alfalaq na qul audhu birabi nnaas]


5.  Kudumu kwa idhkari za asubuhi na za jioni na wakati wa kulala na wakati wa kuamka na wakati wa kuingia na kutoka msikitini na nyumbani na idhkari ya kuingia na kutoka chooni na wakati wa kupanda chombo chochote cha usafiri (kipando).

6.  Atakapotambulikana mwenye kijicho (aliyemdhuru) aamrishwe kutawadha (udhu wa swala) maji yaliyotawadhiwa apewe aliyopatwa na kijicho ili ayakogee.

7. Chakula, vinywaji, mavazi, makazi [nyumba] na mapato yawe yamepatikana kwa njia ya halali moyo ule na thika na  ALLAH  na matumaini makubwa na kunyenyekeya kwa ALLAH  kwa dua na kumtegemea amri ya Subhana wa Taala.

8.  Kuyasomea maji huku  ukiyapulizia na kupewa mgonjwa anywe na yatakayobakia amwagiwe huyo mgonjwa kichwani/mwilini.  


Ukurasa wa Tisa:  

9.  Kutoa swadaka  kwa mafukara  na kuwafanyia ihsaani kadiri iwezekanavyo kutenda hiyo kuna athiri sana  kwa ajili ya kujikinga na balaa ya kijicho na shari ya hasidi.  

10.  Kula punje saba (7) za tende asubuhi ikiwezekana.

11.  Unachukuwa majani saba  ya kijani ya Mkunazi  unayatwanga kwa mawe (kuyaponda) mawili halafu unayatia katika maji kiasi ya kukoga unayasomea maji hayo kwa aya zilizotangulia unakunywa maji hayo mara tatu yatakayo bakia ayakoee na  inshaallah maradhi yatatoka.  Itakapolazimika unawea kurudia mara mbili au zaidi mpaka maradhi yatoke.  Wamejaribu wengi na  wamefanikiwa ni nzuri sana kwa wanaume waliofungwa kwa wake zao.  

12.  unasoma Surati Al Fatiha (Alhamdu),  Aya Kursiyu,  Aya mbili za mwisho wa Sura ya Al Baqara, Sura Ikhlas (Qul- huwa llahu alhad),  Sura ya Al Falaq (qul Aughu bi rabil Falaq), Sura ya Annas (qul- audhubi rabi nnas) x 3 au zaidi huku huku ukipuliia mahali penye maumivu ya mwili.  

13.  Wajibu uliomuhimu ni kumtukuza ALLAH   SUBHANNAHU WA TAALA  kwa kufuata  sheria za dini na Sunnah ya Mtume wake na muhimu kuepuka na SHIRKI  ya aina yoyote.   Matibabu muhimu ya RUQYA  baada ya Qur'ani na Sunnah ya Mtume ni Dua kwa wingi na kutoa Sadaka.  


Imetundikwa hapa leo hii tarehe 3 Aprili, 2015 na mimi  mmiliki wa Blogu hii

Zainab M. Mwatawala.  






 


   





No comments:

Post a Comment