Wednesday, April 22, 2015

AHADI NA DHULMA KATIKA UISLAM

 DAAWA  KWA  WATU

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Mtume (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: 
 ((Allaah Aliyetukuka Amesema: Watu watatu Mimi  Nitakhasimiana nao Siku ya Qiyaamah: Mtu aliyempa nduguye ahadi kwa kutumia Jina Langu kisha akavunja ahadi hiyo. Mtu aliyemuuza muungwana na akala thamani yake. Na mtu aliyemwajiri mwajiriwa naye akammalizia kazi yake, wala asimpe ujira wake)). Al-Bukhaariy

Mafunzo Na Hidaya:

Maamrisho ya kutimiza ahadi
 [Al-Baqarah 2: 177
Al-Maaidah 5: 1]. 

Na asiyetimiza ahadi, atakuwa na sifa ya wanafiki ambao walikuwa hawaachi kuvunja ahadi. 
[Al-Baqarah 2: 100,
 Al-Anfaal 8: 56,
 Ar-‘Rad 13: 25 
[Rejea Hadiyth namba  18].


وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا ﴿٣٤﴾

Na timizeni ahadi; hakika ahadi daima ni ya kuulizwa (Siku ya Qiyaamah) Al-Israa (17: 34)

Kutimiza ahadi ni miongoni mwa sifa zitakazomfikisha Muumin Peponi
 [Ar-Ra’d 13: 20-24,
 Al-Ma’arij 70: 32,
 Al-Muuminuun 23: 8].

Inaruhusiwa kuvunja kiapo kwa kubadilisha jambo ovu kwa jambo jema. [Rejea Hadiyth namba 5].

Allaah (سبحانه وتعالى) Amemsifu Nabii Ismaa’iyl kwa sifa ya kutimizia ahadi [Maryam 19: 54].

Uislamu unahimiza haki baina ya watu na uhuru wa binaadamu.

Makatazo ya kumdhulumu mwajiriwa kwa kutokumlipa ujira wake, kwani kufanya hivyo ni hiana, nayo ni dhulma.


 وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾

Na haipasi kwa Nabii yeyote kukhini. Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. Kisha italipwa kamilifu kila nafsi yale iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa. 
 Aal-‘Imraan (3: 161)

Mtu anayekhasimiwa na Allaah (سبحانه وتعالى), tena Siku ya Qiyaamah, atakuwa katika adhabu kali. Hivyo, ni juu yetu tufanye  yatakayotupatia uhusiano mzuri na Muumbaji wetu, na mambo yote Aliyotukataza tuwe mbali nayo.

No comments:

Post a Comment