Friday, March 27, 2009

UONGEZAJI WA UPEKUZI SAFARI ZA ANGA

A response on passenger Screening Rules being expanded:
Imechangiwa na Bi Saada al-Ghafry.


Hakuna binaadamu anaeweza kukuhakikishia usalama wako
bali Allah peke yake ndiyo mwenye uwezo huo. Watu wengi
zaidi wanakufa barabarani kuliko ajali zote za usafiri hewani,
sikwambii asilimia ndogo kati ya ajali hizo za hewani kuwa
ni waathirika wa kutekwa nyara. Lakini hatuachi kuendesha gari
au kuwa wasafiri kwenye magari. Uthibitishiwe usalama ama
la, malik al mawt akikusimamia huna ujanja...
Mimi nakubali kabisa kuwa ukaguzi ni muhimu. Nimesafiri miaka
nenda rudi kabla ya 9/11 ukaguzi ulikuwepo. Nisichokubali
ni ubaguzi kwenye ukaguzi. Ubaguzi wa kuchagua jina na
rangi.
Niliwahi kusafiri kwenda Tanzania, dakika chache baada
ya kupaa Jeddah, nikasikia mpasuko na ndege ikayumba.
Waliokuwa wamelala wakashtuka. Kila mmoja akawa na
wasiwasi kumetokea nini, mimi niko kwenye dua tu huku
nimemkumbatia mwanangu. Hatimaye tukaelezwa kuwa
injini moja ina matatizo (hatukuelezwa ni matatizo gani).
Hatukuweza kuendelea na safari kuelekea Dar maana
hakuna ufundi, hatukuweza kurudi Jeddah kwa sababu
ya sheria za uhamiaji, ikabidi twende Zurich.
Chuma si lazima kitolewe na abiria mwingine tu. Ndege
nzima ni chuma kinachoweza "kuwaangusha" wakati
wowote.
Tawwakul, Mzee wangu, Tawwakul ndiyo usalama wako.
Likikufika, zako zimefika. Hakuna dawa. Ni sababu tu.

No comments:

Post a Comment