Saba General Bldg. [Inatazamana na Anatouglou, Mnazi Mmoja]
Lumumba Street
DAR ES SALAAM
Simu: 0717 224437; 0785 972626; 0682 677259 au
Wanamume: 0765 462022; 9784 863539; 0713 298114
Wanawake: 0715 273306; 0754 436351; 0715 348009
Madrasat Ruhina
Rahaleo [Nyuma ya Jengo la Radio, Zanzibar
ZANZIBAR:
Simu: Wanamume: 0657 606708; 0777 458075; 0685 366141
Wanawake: 0777 426053; 0777 499918; 0777 428340
Mr. Khalfan Kabbuu [Kidishi]
Macho Manne Traders,
Chake Chake
PEMBA
Simu: 0777 497300; 0773 222542; 0776 357117;
0777513627; 0777429415; 0778682071
Akaunti za Benki:
AHLUS SUNNA WALA JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST
1. Amana bank Tshs.: 001120024610001
USD: 001120024610002
2. PBZ Bank Tshs.: 51120100001378
USD: 51120200001383
3. CRDB Bank: Tshs.: 01J1024740300
USD: 02J1024740300
Ukurasa wa 2
AHLUS SUNNA WAL JAMAA
Tunasimamisha nguzo ya Hijja kuendeleza Uislam
Hadith
"DINI NI NASAHA"
Soma Unasihike
Tuko karibu, tunasali sala 5 katika Misikiti Mitakatifu
GHARAMA ZOTE NI DOLA (USA) 4,500.
Ukurasa wa 3
1. KAMILISHA NGUZO ZA DINI YAKO !
Ewe Muislam, HIJJA NI NGUZO KATIKA UISLAMU, mwenye kuisimamisha amesimamisha Dini. Thibitisha Uislamu wako kwa vitendo upate Radhi za moja wako! Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako na kuanza kufaidi matunda ya Hajj. Karibuni Ahlus Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora.
2. HIJJI, UFE MUISLAMU
Mtume [SAW] amesema kuwa anayekufa bila kuhiji hali ya kuwa aliwahi kupata uwezo anakufa Yahudi au Nasara, na Uislam hautomtambua! Hijja ni haki ya Moja wako iliyopo juu yako! Mpe Mola wako haki yake kwanza kabla ya kufanya mengine.
3. HIJJI UDHAMINIWE NA ALLAH!
Mtume [SAW] amesema kuwa Mwenye kuhiji amedhaminiwa na ni mgeni wa Allah. Tupende sana kwenda kuwa wageni wa Mwenyezi Mungu na kuyaweka maisha yetu katika udhamini (bima) ya Mola Mkarimu. Tulishaitwa sote tangu zama za Nabii Ibrahi (AS), na hakuna wito mwingine binafsi.
4. JEE, UMESHAMZURU MTUME WAKO?
Mtume [SAW] amesema "Mwenye kuja kunizuru baada ya mauti yangu ni kama aliyenitembelea wakati wa uhai wangu". Neema iliyoje kumzuru Mtume [SAW] ! Na huu ni ushahidi wa imani na mapenzi ya muislam. Wewe umeshamzuru Mtume [SAW] mara ngapi? Yako wapi mapenzi yako kama hujamzuru Mtume wako? Karibuni wapenzi wa Mtume [SAW]!
5. TAJIRIKA KWA KUHIJI !
Mtume [SAW] amesema "...Mahujaji wanarudishiwa kila walihokitumia katika Hijja, shilingi moja kwa milioni moja." Hivyo Hijja ni kitega uchumi bora kabisa. Haweza kuwa fakiri abadan mwenye kutekelea Hijja! Karibuni Ahlus Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora.
6. MANUFAA YA HIJJA
Mtume [SAW] anasema, "Mwenye kwenda kuhiji akifa safarini anatiwa Peponi. Akirudi salama kwao anarudishwa na ujira mkubwa na zawadi nyingi". Na akasema tena Mtume [SAW] "Husamehewa mwenye kuhiji na anaowaombea". Twendeni na kupeleka wengine kwa faida ya Umma wa Waislam.
Ukurasa Na. 4
7. AMKA, MUISLAM MTANZANIA !
Unajua kuwa Tanzania tuko nyuma sana katika utekelezaji wa nguzo ya Hijja? Tunakwenda wachache sana, na wengine wetu tukiwa wazee tumeshachoka. Mtume [SAW] amehimiza watu waende Hijja wakiwa vijana wenye nguvu. Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako na uboreshe maisha yako kwa udhamini wa Moja wako.
8. KILA ENEO LIPELEKE MAHUJAJI
Qur'ani imedhamini kuwa tutakwenda Hijja kutoka milima na mabonde ya mbali {Al-Hajj: 27}. Yaani Mwenyezi Mungu [SW] tutoke kila Mkoa, Wilaya, na Mtaa kwenda Hijja kila mwaka. Kila siku tunamuomba Mwenyezi Mungu aboreshe maisha yetu. Lakini sharti lake Allah anataka tuitikie Wito Wake kwanza ! {Al-Baqara: 186} Je? tunaitika?
9. UOMBEZI WA MTUME [SAW]
Mtume [SAW] amesema "Mwenye kuja kunizuru mimi kwa kutaraji ujira kwa Allah, basi mimi nitakuwa muombezi na shahidi wake (siku ya Kiyama)". Neema iliyoje kupata fursa kama hii! Sote tunauhitaji uombezi huu. Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako na kujihakikishia uombezi wa Mtume wako [SAW]. Karibuni wapenzi wa Mtume [SAW] !
10. HASARA ZA KUTOHIJI NI KWETU SOTE !
Allah anasema tuitangaze na kuhimizana kwenda Hijja (Al-Hajj: 27). Kwasababu baadhi yetu wana uwezo na hawaendi Hijja Mwenyezimungu amesema kwa hasira, "Hana haja na viumbe sote" (Aal-Imran: 97). Hivyo, hasara ni yetu sote! Karibuni Ahlus Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora.
Ukurasa wa 5
11. "AL-HAJJ" NI KIPENZI CHA ALLAH !
Katika Ala na Vitakatifu vya Allah ambavyo Ameonya visivunjiwe heshima, bali vitkuzwe kwa faida ya muumin, vingi sana vinapatikana Makka na Madina (Al-Maaidah: 2, Aal-Imran: 96). Umeshaziona alama zake Allah na kujikurubisha kwa Mola wako? Makafiri wanaichukia sana Hijja; kwa hivyo Waislamu tuipende sana!.
12. MTUME ANAHIMIZA !
Mtume [SAW] ameagiza, "Fanyeni haraka kwenda kuhiji!". Tunahimizwa tuende kuhiji tungali vijana ili maisha yetu yadhaminiwe na Allah. Baada ya kupata uwezo, ni makosa kuakhirisha kwenda kuhiji. Masahaba, vijana na wazee, walihiji Hijja nyingi sana. Wewe je? Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako na kufaidi matunda ya Hijja.
13. AFYA, UWEZO NA NAFASI
Tunahitaji afya, uwezo, na nafasi ili kutekeleza Nguo ya Hijja. Rasilimali hizi Ametupa Allah tuzitumie anavyotaka yeye! Hakuna mwenye uhakika wa kufika mwakani Mjuto mjukuu. Unangoja nini? Usimwendekeze shetani (ibilisi). Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako na uboreshe maisha yako kwa udhamini wa Mola wako.
14. WAOKOE WAZAZI WAKO!
Masahaba waliwahijia wazee wao waliokufa bila kuhiji na waliokutwa wamezeeka ilipofaradhishwa Hijja. Hivi sasa waislamu wengine wanakufa bila kuhiji na kuacha mali zaidi ya malipo ya Hijja. Hivyo walikuwa na uwezo wa kuhiji! Uislam hauwatambui wazee hao mpaka wahijiwe! Umeshawaokoa wazazi wako na kuwarudhsia katika Uislamu?
15. MATAJIRI WA KIISLAMU !
Mtume [SAW] amesema "Kutoa katika Hijja ni sawa na kutoa katika Jihadi, shilingi moja kwa mia saba". Uwezo wa baadhi yetu ni uwezo wetu. Waislamu ni kama jengo au kiwiliwili kimoja. Tupelekane Hijja na tusaidiane kuisimamisha nguzo ya Hijja! Kadiri tunavyokwenda wengi Hijja, ndivyo Allah atavyotupa utukufu na nguvu nchini mwetu.
16. TUSHIRIKIANE KUPELEKANA HIJJA !
Wajibu wa kwenda Hijja unawahususu mwenye uwezo na WENYE UWEZO (Aal-Imran: 97). Inawezekana, kwa kuchanga, tukapelekana mmoja mmoja Hijja kila mwaka katika familia, mtaa, msikiti, na kadhalika. Bila shaka Allah atalifurahia hili na atamimina neema kuwa juu yetu. Tuchangishane katika kheri kwa faida yetu sote, Waislamu, tusisubiri, tuchukuwe hatua !
Ukurasa wa 6
17. WAPI KAMA "ARAFA"?
Hijja ni kama Kutano Mkuu wa wailamu wote duniani. Allah anatukusanya sote katika bonde la Arafa ili tujuane na tumiminie Radhi Zake na kuyabariki maisha yetu. Kila mmoja wetu anatakiwa afike hapo angalau mara joja katika umri wake, na ajsikie ndani ya moyo wake kuwa yu miongoni mwa waislamu. Ndugu yetu, wewe umeshahudhuria hapo mara ngapi?
18. KUPATA PEPO KWA SIKU TANO !
Hakuna kitu kinachowalia wenye akili aidi kuliko vipi kuokoka na Moto na kupata Pepo! Hijja peke yake ndiyo inayoweza kumsafisha muislamu na madhambi yote, na akapata Pepo katika muda wa siku tano. Hivyo, hakuna matumizi bora ya fedha, nguvu na nafasi ya mja kuliko kwenda Hijja. Wewe ndugu yetu ushakwenda mara ngapi?
19. HIJJA INAZAA UMOJA NA NGUVU
Hijja inawakusanya waislamu toka kila pembe ya dunia bila kubagua kabila, taifa, wala akida. Hijja ni zoezi na fundisho kubwa la umoja wa waislamu. Allah anatuita huko tukapate manufaa Aliotuandalia (Al-Hajj: 27). Utukufu, nguvu na ushindi ni vya Allah! Twende wengi kutoka kila pembe ya nchi yetu tukapate nguvu zitokazo kwa Allah.!
20. UMESHAWAPELEKA WATOTO HIJJA?
Sahaba mmoja alimnyanyua mtoto wake mdogo na kumuuuliza Mtume [SAW], "Na huyu ananufaika na Hijja?" Mtume [SAW] akajibu "Ndio, na wewe unapata ujira" Wangapi tumewapeleka watoto wetu Hijja? Milioni ngapi tunwatumilia kwa mambo ya fahari? Karibu uwaandikishe watoto na wafanyakazi wako. Karibuni Ahlus Sunna Wal Jamaa, kwa mipango mizuri, huduma bora na uongozi mzuri wa ibada.
GHARAMA ZOTE NI DOLA 4,500
Sheikh Muhammad Dedes
Simu: 0655 462022; 0682 462022; 0777 462022.
Email: muhammad.dedes@yahoo.com
Mwisho wa Kipeperushi
NYIRADI ZA ARAFA BAADA YA KUSWALI DHUHR/LAASIR KUELEKEA QIBLA
BISMILLAHI RAHMAANI RAHIIM
Labayka Allahhumma Labayka
Labayka Laa sharika Laka Labaika
Inna l-hamda, Wanni-mata, Laka walmulk
Laa Sharikika Laka x 3
Laailahailla lahu wahdahu Laa sharikalah
Lahulmulku walahul hamdu yuhyii wayumiitu
Biyaidihi ikhairu wahuwa alaa kulli shai-in Qadiir x 100
Laahaula walaa quwwata illa billahi l-aliyi l-adhym.
Ashhadu annallaha alaa kulli shain qadiiru
Wa annalaaha qad-ahaatwa bikulli shain - ilmaa x 100
Audhu billahi mina sshaitwaani rrajiim
inna llaha huwa ssamiyul-aliim x 3
Kisha SOMA ALHAMDU MPAKA MWISHO x 3
Kisha QULHU WALLAHU AHADU MPAKA MWISHO x 3
Kisha
BISMILLAHI RRAHMAANI RAHIIM
ALLAHUMA SWALI ALLA NNABIYYI L-UMMIYI WARAHMATULLAHI WABAKATUH x 100.
M U O M B E M O L A MTUKUFU M A M B O Y O T E U T A K A Y O.
No comments:
Post a Comment