MAHAKAMA YA KADHI
Written By Mohamed Said on Tuesday, January 20, 2015 | 10:22 AM
[07:00, 20/01/2015] Ally Abubakar:
Sheikh Hamid Jongo |
1.
Leo
kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 11 jioni tulikuwa ktk ukumbi Wa Julius Nyerere
Conference katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala
tukiwawasilisha mapendekezo ya Muswada wa Mahakama ya Kadhi. Tulikuwa taasisi
11: Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Tanzania, Annahar,
Basuta, Tampro, Dumt, Shura ya Maimamu, jumuiya na taasisi mbalimbali kwa
upande mmoja na Bakwata upande wa pili, Tanganyika Legal Society (TLS) nk nk.
Pia alialikwa Jaji Robert Makaramba na Arcado Ntagazwa.
2.
Maoni
ya Jaji Robert Makaramba ni kuwa Mahakama ya Kadhi ni chombo halali na
hakipaswi kuitwa cha kidini bali ni chombo cha dola, kigharamiwe na dola,
Wakristo wasilalamike sababu hata mahakama za kawaida zinatumia sheria za
Kikristo ambazo zinatokana na Common Law.
3.
Bakwata
wao wameiambia Kamati ya Bunge kuwa Mahakama ya Kadhi ni mahakama ya kidini
hivyo isigharamiwe na dola bali zijigharamie zenyewe kama tunavyogharamia
‘’maji ya udhu,’’ ‘’mikeka’’ na ‘’umeme,’’ misikitini, pia Mahakama ya Kadhi
hiyo ndiyo hii Mufti aliyoiunda, na kwamba Mufti anayetajwa na muswada awe ni
Mufti wa Bakwata hiyo iwe rasmi ndani ya sheria. Maoni ya Bakwata
yamewasilishwa na Katibu wa Bakwata Mzee Lolila na Sheikh Hamid Jongo.
4.
TLS
wao wanapendekeza muswada huu uondolewe haufai.
5.
Maoni
yetu ya taasisi 11 kama yalivyoandaliwa na wanasheria kwa ushirikiano na
masheikh yamewasilishwa na Wakili Njama. Kimsingi tumesema huu muswada haufai
uondolewe na badala yake kamati tumeiomba ipokee muswada mbadala tuliouandaa
ambao unaunda Mahakama ya Kadhi, unaunda Bodi ya Sheria za Kiislam ambayo ndiyo
itakayoteua makadhi na kudhibiti nidhamu za makadhi, pia Waziri wa Sheria
asipewe mamlaka ya kutunga sheria au kanuni zinazohusu Waislamu bila ya
kushauriana na wanazuoni. Mahakama ya Kadhi tumetaka iwe sehemu ya “Judiciary,”
igharamiwe na dola. Bakwata na Mufti wa Bakwata wasiwe ndiyo wateuzi wa
makadhi. Tumeitaka Kamati ya Bunge iishauri serikali iuondoe muswada wake
haufai na wala haukidhi vigezo vya kuunda chombo chenye hadhi ya mahakama.
6.
Ntagazwa
ameeleza historia ya Mahakama ya Kadhi na ameeleza kuwa muswada huu hauna nia
ya dhati kuanzisha Mahakama ya Kadhi ya ukweli bali nia ni kupata kura za
Waislamu tu. Ntagazwa aliungana nasi kuwa muswada uondolewe.
7.
TLS
nao waliunga mkono hoja zetu kwa kiasi kikubwa. Katika kikao hicho kwa upande
wetu tulikuwa mimi, Wakili Njama, Dr. Benhajj, Wakili Hamza Jabir,
Masheikh: Kundecha, Kilemile, Sheikh Bawazir, Sheikh Mbalamwezi Mwanahistoria
Mohamed Said na wengi wengine. Alhamdulillah tuliwakilisha vyema na wrote
walituelewa tunaamini kazi tuliitimiza yaliyobaki Allah anajua zaidi. Mjadala
ulikuwa mkali kutwa nzima lakini tuliwatuliza.
[07:00, 20/01/2015] Ally Abubakar:
Aliandika makala Hii ni ndugu ktk Uislam, Mwanasheria/Wakili Juma N.
Dovutwa.
No comments:
Post a Comment