skip to main |
skip to sidebar
Serikali Ya Tanzania Yafuta Kinyemela Mtihani wa Somo la Islamic Knowledge ! ONA MAJANGA !!!
Habari hii imenakiliwa kutoka Jamii Forums, Machi, 2013.
Serikali yafuta kinyemela mtihani wa somo la Islamic !
• Waislam wapanga kumwona Katibu Mkuu - Ikulu !
• Mode hii issue ni very serious nakuomba usiiondoe !
Wana JF,
Habari zenu !
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imepitisha uamuzi wa kutotahini tena mtihani wa somo la Dini ya Kiislam kuanzia mwaka huu
Katika kupitisha uamuzi huo, Wizara ilikutana na taasisi za Kikristo
pekee mwezi machi mwaka huu na baadae kuwapa taarifa Bakwata juu ya
maamuzi yaliyofikiwa.
" Sisi tumefanya tu kupewa taarifa kuwa serikali imepitisha uamuzi huo,
lakini katika kujadili suala hilo hatukufahamishwa, Wizara ilikutana na
wadau wa Kikristo pekee " amesema Afisa mmoja wa Bakwata akieleza juu ya
barua waliyoandikiwa na Kamishna wa Elimu juu ya uamuzi huo.
Afisa huyo akasema kuwa wao kama Bakwata wameshangaa na kushtuka sanaa
Akasema kuwa pamoja na kuwa hawakushirikishwa wanakuja kupewa tu
taarifa, lakini wanashangaa pia kwasababu hata walipopewa taarifa na
Kamishna wa Elimu, wameambiwa jambo hilo liwe SIRI.
Jambo hili linafanywa " SIRI " Je serikali inataka Waislam wasiambiwe ?
Kuna agenda gani ? Amehoji afisa huyo ambaye hata hivyo hakutaka kutaja
jina lake akisema kuwa yeye sio msemaji wa Bakwata.
Awali taarifa juu ya kikao cha Wakristo na Wizara juu ya mitihani ya
dini, zilianza kuvuja kupitia kwa Wakristo waliohudhuria ambao
walipokutana na wadau kutoka upande wa Waislam waliwalaumu ni kwanini
hawakuhudhuria wakasaidiana kupinga uamuzi huo wa serikali.
Hata hivyo, wadau hao kutoka Islamic Education Panel [IEP] waliwafahamisha wadau hao wa Kikristo kuwa wao walikuwa hawakupewa taarifa.
Kufuatia kuvuja kwa taarifa hizo, baadhi ya wajumbe wa Islamic Education
Panel walifuatilia jambo hilo Bakwata wakidhani kuwa huenda wao
walipewa taarifa.
Hata hivyo, maofisa wa Bakwata wakasema kuwa nao wanasikia tu,hawakualikwa.
Kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikitahini masomo ya Dini ya Kiislam (
Maarifa ya Uislam ) na Kikristo ( Divinity )katika mitihani ya kidato
cha nne na sita na pia katika mafunzo ya Ualimu ngazi ya cheti na
Stashahada.
Kwa upande wa Maarifa ya Uislamu, Wizara imekuwa ikishirikisha na
Islamic Education Panel katika kuandaa mihutasari na mitihani kwa ngazi
zote hizo.
Vitabu vya mihutasari hiyo, kwa ngazi zoote, katika jalada vimewekwa
nembo ya serikali na ile ya Islamic Education Panel na kusainiwa na
Kamishna wa Elimu
Hata hivyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, haikuwaita IEP katika
kupitisha uamuzi huo mkubwa wa wenye athari kubwa kwa vijana wa Kiislamu
na Vyuo vya Kiislamu.
Hivi sasa Vyuo Vikuu kama vile Muslim University of Morogoro ( MUM ), pamoja na
wanafunzi wa kozi nyingine, huchukua Wanafunzi waliomaliza kidato cha
sita na kufaulu somo la Islamic Knowledge kwaajili ya kuchukua kozi ya Bachelor of Law & Sharia (sheria na sharia kwa pamoja.)
Aidha, huchukua pia wanafunzi hao kwa ajili ya kozi ya masomo ya Dini na Ualimu, yaaani BA Islamic studies and Education.
Kwa upande mwingine, Chuo kikuu cha Elimu Zanzibar [State University of Zanzibar] - SUZA - ( Chukwani ) na kile
cha Tunguu, navyo vinachukua wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na
kufaulu somo la maarifa ya Uislamu kwa ajili ya kozi zao mbalimbali.
Vipo pia Vyuo vikuu vya Mbale Uganda, Sudan, Uturuki, Malaysia na sehemu
nyingine ambapo wana kozi zinazohitaji somo la Maarifa ya Uislamu kama
vile Islamic Banking.
Kwa uamuzi huu wa serikali, inamaana kuwa sasa itakuwa vigumu kwa MUM na
Chukwani kupata wanafunzi wenye sifa kwahiyo huenda vikalazimika kufuta
kozi hizo.
Hii maana yake ni kuwa uamuzi huu unapunguza idadi ya wanafunzi wa Kiislamu wanaokuwa na sifa za kupata elimu ya juu.
" Hii ni dharau iliyopitiliza kiwango, Serikali inachukuaje maamuzi kama
haya bila kujali kuwa kuna shule za Kiislam na Vyuo vikuu ambavyo
vinategemea kupata wanafunzi kutokana na wanafunzi waliomaliza kidato
cha sita wenye somo la Maarifa ya Uislamu ? "
" Kama Serikali imeona kuna mantiki kujitoa katika kutahini somo hili,
kwanini ifanye kinyemela ? Kwanini isiwashirikishe wadau husika ili
kujua ni utaratibu gani mwingine utafanyika ili Vyuo vikuu vya Kiislamu
vilivyopo visiathirike ? Kwanini wasikae pamoja na Panel ? Mbona
waliwaita Wakristo ? Kitu gani kiliwafanya wakwepe kuwaita Waislamu, ni
dharau , UDINI au kuna agenda gani ya siri ? "
• Mnaiharibu amani ya nchi hii kwa mikono yenu wenyewee.... National Examination Council of Tanzania [NECTA] & SERIKALI yenu sikivu !
The Fixer.
No comments:
Post a Comment