POSTED HERE FROM www.alhidaaya.com on 8/1/2013
WASIYA WA KISHARI'AH WA
MUISLAMU KABLA HAJAFARIKI
(Mfano Wa Wasiya Ambao
Muislamu Anaweza Kuuandaa Na Kuwa Nao Nyumbani Tayari Akijiandaa Na Mauti)
بسم الله الرحمن الرحي
www.alhidaaya.com
((وَاتَّقُواْ يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى
اللّهِ ثُمَّ تُوَفَّى كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لاَ يُظْلَمُونَ))
((Ogopeni Siku Ambayo Mutarudishwa Kwa Allaah Kisha Kila Nafsi
Italipa Kila Lile Ililochuma Na Wao Hawatadhulumiwa)) (Al-Baqarah: 281)
Utangulizi
Shukrani zote Anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu wote. Swalah
na amani ziwe juu ya aliyetumwa awe ni Rehma kwa ulimwengu wote Mtume Muhammad
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم , Ahli zake, Swahaba na wale ambao wamefuata Sunnah
zake mpaka siku ya mwisho.
Nimefikiri kuhusu mauti mara kadhaa na nimejaribu sana kule
kukutana kwangu na Allaah سبحانه
وتعالى kuwe ni kwenye kumridhisha na kuwe
mbali na uzushi wa zama hizi. Nami nina yakini kabisa kuwa kila bid’ah (uzushi)
ni upotevu na kila upotevu malipo yake ni moto. Na pia kila uzushi ni upotevu,
japokuwa watu watayaona ni mazuri na mema.
Nimesoma mengi kuhusu janaza na wasiya wa kishari’ah lakini
sijapata kilicho kamilika wala bora kuliko kitabu “Hukumu ya Janaza na
Uzushi wake” cha Shaykh Muhammad Naaswirud Diyn Al-Albaaniy Allaah سبحانه وتعالى
Amrehemu.
Ewe ndugu yangu… Tukumbuke mauti daima… Mpaka tufanye amali ya
baada ya mauti. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema:
((أكثروا
من ذكر هادم اللذات..()
((Zidisheni katika kukumbuka mauti)) [At-Tirmidhiy, Ahmad na Ibn
Maajah]
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesisitiza kuhusu kuacha wasiya ulioandikwa, akasema:
((ما
حق إمرئ مسلم يبيت ليلتين وله شئ يوصى فيه إلا ووصيته مكتوبة عند رأسه))
البخارى ومسلم
((Ni haki gani ya Muislamu anayekaa masiku mawili na ana kitu
cha kukitolea wasiya ila na wasiya wake umeandikwa chini ya kichwa chake))
[Al-(Bukhaariy
na Muslim]
Wasiya Wangu Wa Kijumla
Watu wa nyumbani kwangu watukufu, nawausia:
1) Mpwekesheni Allaah سبحانه وتعالى Pekee (At-Tawhiyd)
na mujihadhari na kuingia katika kumshirikisha. Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
((إِنَّ
اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ
وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَن يَشَاء .... ))
((Hakika Allaah Hasamehe dhambi za kushirikishwa, na Anasamehe
dhambi lisilokuwa hilo kwa Amtakaye…)) [An-Nisaa 4: 48, 116]
2) Muogopeni na kumpenda Allaah سبحانه وتعالى na mufuate Shari’ah zake
kwa siri na dhahiri. Hifadhini nguzo za Uislamu, amrisheni mema na mkatazane
mabaya, ungeni ujamaa na kizazi na mushikamane na kila kitukufu na twa’a ya
Allaah سبحانه وتعالى Aliyetukuka na fuateni Sunnah za Mtume Wake صلى الله عليه وآله وسلم.
3) Nawausia mfanye tawbah ya kweli kweli na sawa kutokana na kila
maovu na maasi na ombeni maghfirah (msamaha), mkumbukeni na mumtaje
Allaah سبحانه وتعالى kwa wingi na muisome Qur-aan kila mchana na usiku.
4) Nawausia muwe na subira na kuridhika wakati wa msiba mara ya
kwanza na museme:
إنا لله وإنا إ ليه راجعون اللهم أجرنا فى مصيبتنا واخلف لنا خيرا
منها
“Bila shaka tunatoka kwa Allaah سبحانه وتعالى na Kwake ndio marudio. Ee Allaah Tupe ujira katika msiba wetu huu
na Utubadilishiye lililo bora zaidi kuliko huo msiba.”
5) Msinitangaze katika magazeti wala vipaza sauti bali wasilianeni
na jamaa zangu na marafiki ili wanioshe na kuniswalia….Na kunivisha sanda na
kuniombea Du‘aa pamoja na kuniombea maghfirah (msamaha).
6) Msikae sehemu ya msiba…wala katika hema au nyumba za sherehe au
kumbi za kukodisha au nyumba za kawaida. Haikuonekana kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala
Maswahaba wala Tabi’iyn kuwa wamekusanyika katika msiba baada ya kuzikwa.
7) Na msiba katika Shari’ah ya Allaah سبحانه
وتعالى Na Sunnah ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni
kumsomea mtu wakati wa kukata roho “La ilaaha illa Allaah”. “Hapana mungu anayepasa kuabudiwa kwa haki ila Allaah”. Na kisha kumwosha,
kumvisha sanda, kufuata jeneza lake, kumzika na kungojea saa baada ya kuzika
kwa kumuombea du‘aa na maghfirah maiti. Amesema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na
yeye akiwa kwenye mazishi kaburini:
((استغفروا
لأخيكم وسلوا له التثبيت فإنه الآن يسأل))
((Muombeeni
maghfirah ndugu yenu na mumtakiye uimara (kutoyumba) kwani sasa
anaulizwa)) [Abu
Daawuud]
Na hivyo hivyo muwatayarishie chakula watu walio na msiba
(waliofiliwa). Huu ndio utaratibu wa msiba wa kishari’ah na kinyume na hayo ni
uzushi (bid’ah).
8) Msinililie kwa sauti….Wala msiyahesabu mazuri yangu. Wala
msilie kwa sauti kubwa…wala msikwaruze nyuso zenu. Wala msizichane nguo... wala
msijipige.
9) Kunakatazwa kabisa ada zote za uzushi kama kukusanyika
Alkhamiys, arobaini, au baada ya maiti kutimiza mwaka, au siku za ‘Iyd na
kujiliza na sherehe za wakati mbali mbali. Msisome Qur-aan kwenye makaburi wala
msigawanye Swadaqah na wala msichinje chochote chini ya Jeneza.
10) Kwa jamaa zangu na marafiki wapendwa wanilipie madeni kabla ya
kuoshwa na kukafiniwa (kuvishwa sanda) na watekeleze nadhiri zangu.
11) Nawausia watoto wangu, msiba na huzuni usizidi siku tatu. Na
kwa mke wangu msiba ni miezi minne na siku kumi. Na asivae kwa wakati huo
hariri wala nguo za rangi au asitie wanja, mafuta na asijipambe.
12) Pia nawausia watoto na jamaa zangu wazuru kaburi langu,
waniombee du’aa pamoja na kuniombea maghfirah. Hii itawasaidia kupata
mazingatio na mawaidha katika mauti.
13) Vivyo hivyo nawausia watoto, jamaa, marafiki na watu wa
Msikiti wanikumbuke kwa wema, na kuniombea du’aa na kunitakia maghfirah
katika wakati wa Swalah zao kwa Allaah سبحانه وتعالى Wanaposujudu, baada ya
Swalah na kusoma Qur-aan tukufu… Wakati wanapohiji kwenye nyumba tukufu ya
Allaah ili Allaah Aniondolee adhabu ya kaburi na adhabu ya moto wa Jahannam na
Aniingize kwa Rehma Yake peponi.
14) Inaruhusiwa kwa mke wangu (na kinyume chake) kuniosha na
kunikafini.
15) Inaruhusiwa kungojewa kwa mzazi au mtoto mpaka afike kwa muda
unaongilika akilini.
16) Inawezekana kuniswalia kwenye makaburi kwa yule aliyekosa
Swalah ya Jeneza kabla ya kupita mwezi baada ya kuzika.
17) Gawanyeni kopi za wasiya kwa waliohudhuria mazishi na Swalah
punde tu wanapoingia ili wapate kusoma na kutekeleza yaliyo ndani ya wasiya.
18) Ninawapatia habari kama nimemsamehe kila mwanaadamu aliye na
haki yangu na ninawaomba nilio na haki zao wanisamehe.
19) Jueni kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema:
((ينقطع
عمل ابن آدم من الدنيا إلا من ثلاث : صدقة جارية أو علم ينتفع به أو ولد صالح يدعو
له))
((Amali ya binadamu hukatika baada ya kufa ila kwa mambo matatu:
Swadaqah yenye kuendelea, elimu yenye manufaa au mtoto mwema anayemuombea)) [Muslim na Ibn Maajah].
20) Ninawaageni kwa jina la Allaah Ambaye mwagano wake haupotei.
Wakati Wa Kutoka Roho
Enyi wapenzi wangu!
Wakati unapokaribia wa kukata roho waiteni watu wema. Wahesabuni
hivyo, wala simtakasi yeyote mbele ya Allaah.
Jina
|
Simu
|
Jina
|
Simu
|
|
|
|
|
Wakati Wa Kukata Roho
Enyi vipenzi vyangu:
1) Msiwe na wasiwasi na msubiri kwani napenda kukutana na Allaah
na kuweni na dhana nzuri. Na nisomeeni kalimah ya Tawhiyd, “La ilaaha illa Allaah” kwa ulaini na upole mpaka
hayo yawe maneno ya mwisho ya kukutana na Mola wangu. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
amesema
((من
كان آخر كلامه لا إله إلا الله دخل الجنة))
((Yeyote yatakayokua maneno yake ya mwisho La illaah illa
Allaah ataingia peponi))
2) Nifungeni macho... Na museme Khayr (wema) kwani Malaika
wanaamini munayosema:
اللهم اغفر له .. وارحمه..
وارفع درجته فى المهديين المقربين..
واخلفه فى عقبه فى الغابرين..
واغفر لنا وله يا رب العالمين..
وافسح له قبره.. ونور له فيه.
“Ee Mola Msamehe… na
Umrehemu…Muinue daraja yake awe wa karibu walioongoka… Wabadilishie kizazi
chake kwa yaliyopita…Na Utusamehe sisi na yeye. Ee Mola wa Ulimwengu…Mpanulie
kaburi lake…na Umtilie mwangaza.
3)
Nifunikeni kikamilifu na mnisitiri mwili wangu mzima.
4) Na ikiwa nimehirimia kwa Hijjah au Umrah, basi msinifunike
kichwa, uso wala msinitie manukato.
5) Na nikiwa niko katika vita vya Jihaad, basi asinioshe yeyote,
bali niacheni na nguo zangu hizo na nizikeni na damu yangu.
6) Msinielekeze Qiblah na niacheni katika hali yangu hiyo wala
msinisomee Qur-aan.
7) Nizikeni katika sehemu ambayo itakua rahisi kwenu.
8) Nilipieni madeni kabla ya kunikafini kutoka kwa mali yangu
mwenyewe. Ikiwa sina mali basi waulizeni watu wa kheri katika jamaa na marafiki
zangu… Allaah Atawajaza (Atawapa) kila la kheri. Ikiwa hawatapatikana basi
Allaah Aliyetukuka Atanilipia deni langu.
Wakati Wa Kuoshwa
1) Asihudhurie kuoshwa kwangu ila mwaminifu na aliye mwema.
2) Nisitirini wakati wa kuoshwa tupu yangu kutoka kitovu mpaka
magoti.
3) Mwanzo nitoeni najasa. Kisha ziosheni viungo vya Wudhuu na
mwili wangu wote kwa maji na sabuni.
4) Kisha nitieni Wudhuu wa Swalah kwa maji twahara lakini
msiingize maji kwenye mdomo wala pua yangu. Kisha utieni mwili wangu kwa maji
twahara mara tatu au tano… au saba.
5) Kisha nitieni maji ya waridi (marashi) kwenye nywele na vitanga
vya mikono na sehemu zinazosujudu baada ya kumaliza kuniosha na kukauka.
6) Nivisheni bafta (kitambara) tatu nyeupe na mtie manukato baina
yake na munistiri uso na miguu yangu.
7) Na ikiwa nimekufa shahidi katika vita basi asinioshe yeyote,
niacheni na nguo hizo na munizike (nilivyokufa) na damu (kama imetoka).
Swalah Ya Jeneza
Imaam wa Swalah hiyo ni…………………………… au awe ni mtu yeyote mwema.
Swalah ya maiti (au Jeneza) ina takbiyr nne:
1. Utasoma Suratul Faatihah baada ya Takbiyr ya
kwanza.
2. Kisha du’aa ya Ibraahiym عليه السلام baada
ya Takbiyr ya pili yaani,
(اللهم
صلى على محمد ...)
“Allaahumma swali ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad kama
Swallayta ‘alaa Ibraahyima wa ‘alaa aali Ibraahiym…” mpaka mwisho baada takbiyr
ya pili.
3. Na mniombee baada ya takbiyr ya tatu.
اللهم إنا جئناك شفعاء له .. فشفعنا فيه
اللهم اغفر له وا رحمه .. وعافه واعف عنه
وأكرم نزله .. ووسع مدخله
وأغسله بالماء والثلج والبرد ..
ونقه من الخطايا كما ينقى الثوب الأبيض من والدنس
وأبدله دارا خيرا من داره .. وأهلا خيرا من أهله
وزوجا خيرا من زوجه وأعذه من عذاب القبر وعذاب النار .
اللهم أبدل سيئاته حسنات
اللهم إن كان مسيئا فتجاوز عن سيئاته
Allaahumma inna ji-inaaka shufa’a-an lahu fashfi‘na fiyhi.
“Ee Mola sisi tumekuja kwako kumuombea Shafa’a
basi mpatie Shafa’a”
Allaahumma ghfir lahu warhamhu wa ‘afihi waa‘fu ‘anhu
“Ee
Mola Mghufirie na Umrehemu”.
Wa akrim nuzulahu wa wasi‘i mudkhalahu.
“Na Ukirimu kushuka kwake na Yapanue maingilio yake”.
Waaghsilhu bilmai wath-thalji walbard. Wanaqih minal Khatwaaya
kama yunaqqath-thawabul abyadhw minad-danas. Wa-abdilhu daaran Khayran min
daarihi wa ahlan khayran min ahlihi. Wazawjan khayran min zawjih Wa a ‘idhhu min adhabil Qabr
wa adhaabin-naar Allaahumma abdili sayyiatahu hasanaat. Allaahumma in Kaana
musiy-an fatajawaz ‘an sayyiatihi.
‘Na muoshe kwa maji, theluji na ubaridi (barafu)’ Na yasafishe
makosa yake kama inavyosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu. Na mbadilishie
nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake. Ikiwa
anayeswaliwa ni mwanamke basi maneno haya hayatajwi (Na mke bora kuliko wake).
Na mwepushe na adhabu ya kaburi na adhabu ya moto. Ee Mola mbadilishie makosa
yawe ni thawabu. Na akiwa ni muovu basi yasamehe maovu yake.
4. Baada ya takbiyr ya nne soma du‘aa ifuatayo:
االلهم لا تحرمنا أجره ولا تفتنا بعده واغفر لنا وله وللمسلمين .
Allaahumma laa tahrimnaa ajrahu walaa taftinnaa ba‘adahu
waghfirlanaa walahu walilmuslimiyn.
‘Ee
Mola Usituharamishie ujira wake wala Usitufitini baada yake na Utusamehe sisi
na yeye na Waislamu wote’.
Katika Kulichukua Jeneza
1) Liharakisheni Jeneza langu enyi wapenzi wa Mtume wa Allaah.
2) Na nyamazeni kabisa katika Jeneza kama kwamba katika vichwa
vyenu kuna ndege.
3) Wala wasifuate Jeneza langu wanawake.
4) Wala asilie yeyote kwa sauti…
5) Subira wakati wa msiba mkubwa. Na kubwa zaidi ya hiyo kuna
ujira wa ridhaa katika Qadhaa (hukumu) ya Allaah yote… kheri na shari…
Tamu na chungu.
(قل
كل من عند الله فمال هؤلاء القوم لا يكادون يفقهون حديثا)
((Sema: Yote yanatokana na Allaah Basi wana nini watu hawa hata hawakaribii kufahamu
maneno?)) An-Nisaa: 78
6) Kueni wanyenyekevu wakati wa Jeneza mkitafakari jambo hili
kubwa la mauti. Wala musizungumze kwa hadithi za dunia na musifanye dhihaka.
Musiseme pia, “wahhiduhu” ‘mpwekesheni’ au “Astaghfiru Allaah”.
Na amkumbuke Allaah yule mwenye kuchukua Jeneza.
6) Msiguse Jeneza kwa mikono, vitambara au vitu vingine kwa Niyyah
ya kujipata baraka; Hii ni haraam.
Wakati Wa Kuzika Na Baada Yake
1) Mnapoingia kwenye makaburi semeni:
Assalaamu ‘alaykum daara qawmin muuminiyna antum saabiquuna wa
ghadan in shaa Allaah nahnu bikum laahiquun. Nas-alu Allaah lana walakumu
l’aafiya.
“Amani iwe juu yenu nyumbani mwa watu waumini Nyinyi mumetutangulia
na sisi kesho Anapopenda Allaah tutakua ni wenye kuwafuatia.
Tunamuomba Allaah Atupatie sisi na nyie.
2) Enyi watu, wanizike marafiki zangu walio wema. Mnaponiingiza
kaburini semeni:
(بسم
الله وعلى سنة رسول الله)
“BismiLlaahi wa ‘alaa Sunnati Rasuuli Allaah.”
Kwa jina
la Allaah na kwa Sunnah ya Mtume wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم
3) Enyi wapenzi wangu, marafiki na ndugu zangu katika imani ambao niliwapenda
duniani kutafuta radhi za Allaah. Msiniache peke yangu wakati huu ambao nina
haja kubwa nanyi. Kaeni pamoja nami kwenye kaburi kiasi cha kutosha huku
mkiniombea du‘aa Allaah Atawaruzuku mwenye kuwaombea du’aa mnapokufa.
Allaah Awalipe wote…
Msiba wa kishari’ah umemalizika kwa kulifuata Jeneza na wala
hakuna msiba kabisa kwa wanawake….Allaah Awarehem
4) Mimi niko mbali na maneno au vitendo vinavyokwenda kinyume na
Shari’ah ya Allaah na Sunnah ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم.
5)
Muogopeni Allaah mwisho wa kumuogopa na sikilizeni na kutii na muwe na hadhari
na maneno ya Allaah Aliyetukuka:
((إِنَّ
الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَى مِن بَعْدِ مَا
بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ أُولَئِكَ يَلعَنُهُمُ
اللّهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ))
((إِلاَّ
الَّذِينَ تَابُواْ وَأَصْلَحُواْ وَبَيَّنُواْ فَأُوْلَئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ
وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ))
((Hakika
wale wanaoficha Tuliyoyateremsha nazo ni hoja zetu zilizo wazi na uongozi, baada
ya Sisi kuzibainisha kwa watu kitabuni, hao Anawalaani Allaah, na wanawalaani
kila wenye kulaani))
((Ila
wale waliotubu na kutengeneza na kubainisha, basi hao Nitawapokea na Mimi ni
Mwenye kupokea toba na Mwenye Rehema)) (Al Baqarah: 159-160).
8) Zingatieni maneno ya Allaah:
((أَلاَّ
تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى)) ((وَأَن
لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلاَّ مَا سَعَى)) (( وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ
يُرَى)) ((ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاء الْأَوْفَى)) ((وَأَنَّ
إِلَى رَبِّكَ الْمُنتَهَى))
((Kwamba
haichukui nafsi dhambi za nafsi nyengine)) ((Na kwamba mtu hatapata ila yale
aliyoyafanya)) ((Na kwamba ‘amali yake itaonekana)) ((Kisha
atalipwa malipo yaliyo kamili)) ((Na kwamba mwisho unarejea kwa Mola
wako)).
(An-Najm: 38-42)
Wasiya Wangu Wa Mwisho
“Inafaa
kwa Mwenye kuusia, kuusia thuluthi ya alivyoacha kwa mwenye kupenda.”
1) Nawausia mugawe mirathi kulingana na Shari’ah ya Allaah na
yenye kumridhisha Yeye na kuweni enyi vipenzi vyangu ni wenye kupendana nyinyi
kwa nyinyi. Na pendaneni na wapatieni wenzenu nafasi ya mwanzo ingawa hali zenu
ni ndogo. Kila mmoja atapitia njia hii ya mauti kama mimi. Fanyeni ‘amali kwa
siku hii, mutapata furaha kukutana na Allaah mukiwa katika hali ya amani na
utulivu. Siku ya Qiyaamah Ataita Allaah Aliyetukuka:
((أين
المتحابون بجلالى ؟ اليوم أظلهم فى ظلى يوم لا ظل إلا ظلى))
(رواه مسلم)
((Wawapi
waliopendana kwa ajili ya Utukufu wa Allaah leo nitawaweka kwenye kivuli Changu
siku ambayo hakutakuwa na kivuli ila kivuli Changu)) [Muslim]
2) Kuweni karibu na mama yenu[1]