Imechangiwa na Baajun Tambiko (sbaajun@yahoo.com)
Data zako zinazoonyesha wasomi wengi kati ya Wayahudi milioni 14 (14m) kuliko Waislam bilioni mbili na nusu (2.5b) duniani zina ukweli. Na Ujumbe wako ni muhimu sana. Lakini pamoja na hayo tafsiri ya data hizi ni lazima zichambuliwe kwa undani; kama ifuatavyo:
Data zako zinazoonyesha wasomi wengi kati ya Wayahudi milioni 14 (14m) kuliko Waislam bilioni mbili na nusu (2.5b) duniani zina ukweli. Na Ujumbe wako ni muhimu sana. Lakini pamoja na hayo tafsiri ya data hizi ni lazima zichambuliwe kwa undani; kama ifuatavyo:
Kwanza wa-Jew wengi waliotajwa kwenye mchambuo huu, wana-asili ya Central Europe na Western Europe. Hivyo maendeleo yao mengi yanatokana na maeneo waliyoishi na sio dini yao. Na waJew wengine waliotolewa mfano kwenye article kama Karl Marx, Segmund Freud, n.k walikuwa Atheist (watu wasioamini Mungu). Hivyo uJew wao ulikuwa wa ukabila na sio wa dini. Hivyo tunapofanya mlingano ni lazima tulinganishe chungwa kwa chungwa na apple kwa apple.
Na kwa historia tu, waislamu walipokuwa wanatawala Spain, waliweza kuanzisha vyuo vikuu ambavyo vilitia chachu katika maendeleo ya sasa ya elimu yaliopo katika nchi za Magharibi. Na kwa mtaji huu dini ni imani na inatakiwa kupokelewa na mtu wa aina yoyote yule. Kwa upande mwingine elimu si imani, na maendeleo yake yana vigezo vingine ikiwemo sehemu watu wanayoishi. Na kama maendeleo ya elimu hayajali maeneo basi Ethiopia ingekuwa moja ya nchi iliyoendelea maana Jews wameishi Ethiopia toka zama za Nabii Suleiman.
Naomba nieleweke kuwa maelezo yangu sio ya kutafuta visingizio kwanini tupo nyuma kielimu. Maelezo yangu ni kutaka kusema kuwa ELIMU HAISHUKI kutoka mbiguni. Elimu inaambatana na maendeleo ya utawala ulio bora. Elimu inaambatana na maendeleo ya kiuchumi na vile vile usalama wa jamii. Himaya za KiIslamu zilipokuwa na utawala wa bora wenye kuhimiza maendeleo ya Elimu na maendeleo, waIslamu walifanya vizuri.
Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, nchi nyingi zimepata uhuru. Na zile nchi zilizojaribu kuleta maendeleo kwa watu wao matokeo yanaanza kuoneka. Na kuhakiki points zangu nitatumia article uliyotumia. Article hiyo inasema kuwa, katika vyuo 500 bora hakuna vyuo katika nchi za kiIslamu. Kwa miaka ya hivi karibuni usemi huu sio sahihi. Vifuatavyo ni vyuo vikuu katika nchi za Kiislamu vilivyo katika list ya 500 na nafasi zake. (http://www.topunive rsities.com/ university_ rankings/ results/2008/ overall_rankings /fullrankings/)
230 - Universiti MALAYA (UM) Malaysia
287 - University of INDONESIA Indonesia
313 - Universiti Sains MALAYSIA (USM) Malaysia
316 - Universitas GADJAH MADA Indonesia
320 - Universiti Putra MALAYSIA (UPM) Malaysia
338 - KING FAHD University of Petroleum & Mine... Saudi Arabia
374 - BILKENT University Turkey
376 - ISTANBUL Technical University Turkey
376 - National University of Sciences and Tech... Pakistan
287 - University of INDONESIA Indonesia
313 - Universiti Sains MALAYSIA (USM) Malaysia
316 - Universitas GADJAH MADA Indonesia
320 - Universiti Putra MALAYSIA (UPM) Malaysia
338 - KING FAHD University of Petroleum & Mine... Saudi Arabia
374 - BILKENT University Turkey
376 - ISTANBUL Technical University Turkey
376 - National University of Sciences and Tech... Pakistan
Vingine katika orodha ni:
CAIRO University Egypt
University of LAHORE Pakistan
SABANCI University Turkey
AIRLANGGA University Indonesia
BOGOR Agricultural University Indonesia
University of BRAWIJAYA Indonesia
CUKUROVA University Turkey
University of DHAKA Bangladesh
DIPONEGORO University Indonesia
HACETTEPE University Turkey
University of KARACHI Pakistan
SHARIF University of Technology Iran
University of Engineering & Technology (... Pakistan